Mikate Ya Maji Ya Chumvi

Mikate Ya Maji Ya Chumvi 

  

 

Vipimo: 

Unga wa ngano -  2 vikombe (mugs)  

Mayai -   2

Chumvi -  Kiasi

Kitunguu maji cha kiasi -  1

Kotmiri -  2 misongo (bunch)

Mafuta au samli ya kupkia -  Nusu kibakuli

Maji -  3 Vikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Tia maji na mayai kwanza katika mashine ya kusagia (blender) kisha
  2. Tia unga, chumvi usage ili unga uchanganyike.
  3. Mimina katika bakuli, ikiwa unga mzito, ongeza maji kama   uwe mwepesi kiasi.
  4. Katakata kitunguu maji na kotmiri uchangaye.
  5. Weka kikaango kisichoganda (non-stick frying pan) katika moto na uteke unga kwa upawa wa duara uutandaze vizuri katika kikaango.
  6. Subiri mkate ukauke, ugeuze upande wa pili huku unaungandamiza na kuuzungusha mkate katika kikaango ili uive.
  7. Uinue kidogo utie kijiko kimoja cha supu, mafuta au samli.
  8. Kakaanga hadi mkate uive uwe rangi ya hudhurungia kama katika picha.
  9. Geuza tena mkate na ugandamize gandamize tena kama dakika moja uive vizuri upande wa pili bila ya kutia tena mafuta kisha epua uweke katika sahani. Au unaweza kuukunja kama katika picha.
  10. Endelea kupika mingine hadi umalize.

Kidokezo :

Mizuri  kuliwa na asali.

 

 

 

Share