Skip to main content

Chapati Kavu Za Hamira

Chapati  Kavu Za Hamira

Vipimo

Unga - 6 gilasi

Maziwa ya unga - 2 vijiko vya supu

Hamira - 2 vijiko vya chai

Mafuta

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka vitu vyote katika bakuli kisha changanya na kanda kwa maji hadi uwe laini kama unga wa chapati.
  2. Fanya madonge madogodogo.
  3. Uache uumuke.
  4. Sukuma kama chapati, kisha choma kwenye mkaa kwa kuweka wavu juu ya makaa au katika chuma (frying pan).
  5. Geuza pande zote mbili kuwivisha.