Mwanamke Kujichezea Hadi Apate Matamanio Afanye Ghuslu?

SWALI:

mimi nina swali kuhusu upungufu wa udhu. vitu gani vinavyo punguwa udhu wa mtu na vinavyomfanya aoge

kama mwekujitoa najsi? hata mwanamke akijicezesha mwenyewe mpaka kufika kwenye kutaka kuonana na mwanaume alakini asionane nae, navyenyewe vinatowa udhu wake? je akijiingiza vidole katika tupu lakenivilevile nayo ni najsi?


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa muuliza swali hili kuhusu wudhuu na Ghusl. Lakini kabla ya kujibu tungependa kuomba ndugu na dada zetu wanaotuma maswali yao wawe ni wenye kuandika kwa mfumo wenye kueleweka ili tusiwe ni wenye kuyarudisha kwenu ili tupate ufafanuzi wa ziada. Kufanya hivyo kutawachelewesha nyinyi kupata majibu yenu.

Ama kuhusu vitu vinavyovunja wudhuu ni kama yafuatayo:

  • Kutokwa na mkojo, kinyesi au upepo katika sehemu ya siri.

  • Kutokwa na manii, madhii na wadii.

  • Kulala kwa namna ya kutofahamu chochote.

  • Kurukwa na akili kwa kulewa au uwenda wazimu.

  • Kushika uchi wa mbele pasi na kizuizi.

  • Kula nyama ya ngamia.

Ama kuhusu mambo yanayomlazimu Muislamu kuoga mwili mzima (Ghusl) kwa namna tuliyofundishwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni yafuatayo:

  • Kutokwa na manii katika hali yoyote ile.

  • Kujamiiana kwa mume na mke hata kama hawakushusha.

  • Kutokwa kwa damu ya hedhi na nifasi.

  • Kusilimu kwa kafiri.

Ikiwa mwanamke atajichezea kwa njia yoyote ile atakuwa na madhambi kwani hiyo ni njia iliyokatazwa na Uislamu. Kuijisugua hakufai kwa mwanamme wala mwanamke. Mwanamke Muislamu anafaa ajiepushe kujipeleka katika kufikia hali hiyo. Ni jambo lenye kufahamika kuwa yapo madhara mengi yanamfikia mwenye kucheza cheza na sehemu zake za siri. Dhara kubwa ni lile ambalo linamfanya yeye asifae pindi anapooa au kuolewa.

 

Lakini ikiwa kwa kucheza cheza huko atatokwa na manii basi itabidi aoge josho la janaba kabla ya kutekeleza ‘Ibaadah ya Swalah. Ikiwa kujichezea kutakuwa ni juu ya nguo na akafika hadi kwa ile raha anayoiona kutaka kukutana na mwanamme huko hakutomvunjia wudhuu wake kabisa ila tu kama atatokwa na madhii. Ama ikiwa mwanamke atatia vidole vyake katika sehemu zake za siri wudhuu wake utavunjika na itabidi achukue wudhuu kwa ajili ya Swalah.

Soma maswali na majibu katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi ya makatazo ya aina hayo:

Nini Hukumu Ya Kujichua Sehemu Za Siri Au Kujisaga?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share