Damu Ya Hedhi Inayotokeza Na Kurudi Vipi Kuhusu Swawm Afunge Au Asifunge?

Damu Ya Hedhi Inayotokeza Na Kurudi Vipi Kuhusu Swawm Afunge Au Asifunge?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI: 

 

Tafazalini naomba muni fafanuliye aya yafuatayo.

Nikiwa kati ya hali ya kike kuna muda damu inasima kisha tena inarudi kutoka. na hali hii ina nisumbuwa sana kama tuko katika huwu mwezi wa ramadhani. Mathalani kawaida huwa na fanya siku 4 lakini hapa kati kuna siku 1hedhi in kuwa imesima sasa hiyi siku yenye imesimama nitafanya aje nitafunga ama nitasubiri nijitwaharishe?

 

Nina shukuru kwa yote.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kuhusu swali lako yapo mambo ambayo tunafaa tuyaangalie ili tupate hukumu muafaka. Mambo yenyewe ni kama yafuatayo:

 

1-Utajaribu kwanza kutofautisha baina ya damu yako ya hedhi na damu nyengineyo, utaangalia hii damu ikiwa rangi, harufu na twabia (maumbile) yake ni kama ya hedhi au ni tofauti. Ikiwa ni kama ya hedhi basi utabaki umekatazwa kuswali, kufunga na kujimai na mumeo kama ulivyokuwa kwani hakuna muda maalumu wa mwisho wa hedhi, ingawa ‘Ulamaa wengine wameweka mpaka wa siku kumi na tano (15). Ukipata damu ni kinyume na kawaida ya hedhi yako, utaoga na kuswali kwani hiyo haitakuwa ni ada ya hedhi yako.

 

2-Ikiwa huwezi kutofautisha baina ya hedhi na damu nyengineyo, na jambo hili linapatikana kwa wanawake wengi, utabaki katika hali ya hedhi. Hivyo, hutaswali, hutafunga wala kujamiiana na mumeo mpaka utwahirike kwani hakuna mipaka ya muda kwa damu ya hedhi.

 

3-Ama ule umanjano na kufifia kwa rangi ni maji anayoona mwanamke kama usaha na umanjano wake umeiva. Mwanamke anapoona hii baada ya kukatika damu au baada ya kukauka, haichukuliwi kuwa ni hedhi, naye atakuwa twahara. Kwa hiyo, ataswali, atafunga na kuweza kujamiiwa na mumewe. Hiyo ni kwa mujibu wa Hadiyth ya Umm ‘Atwiyah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) aliyesema: “Tulikuwa hatuchukulii fifia kwa rangi na umanjano chochote” [Abu Daawuwd, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah]

 

Kwa maelezo zaidi bonyeza viungo vifuatavyo upate maswali na majibu yenye mas-ala kama haya:

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Fataawaa: Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

Damu Ya Hedhi Inayoendelea Kwa Muda Mrefu

 

Istihaadhwah (Damu Inayoendelea baada ya Hedhi) Na Hukumu Zake

 

 

Na Alaah Anajua zaidi

 

 

Share