Kumuadhinia Maiti Anapozikwa Inajuzu?

 

Kumuadhinia Maiti Anapozikwa Inajuzu?

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Wakati wa kuzika maiti watu wengine wanawa adhiniya maiti inafaa.

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Haifai Muislamu kuadhiniwa kaburini au nje yake anapoaga dunia. Haikupatikana kabisa dalili ya kufanya hivyo katika mafunzo ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida zaidi:

 

Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti

 

Yampasayo Maiti

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share