Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 08

 

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislaam - 08

 

Imefasiriwa na: Naaswir Haamid

 

Alhidaaya.com

 

 

Suala Nambari 8 Linaloeleweka Vibaya

 

Uislaam haustahamilii dini nyengine kwasababu:

 

  • Qur-aan inalaumu dini nyengine kuwa ni za uongo

 

Allaah Ametufundisha ndani ya Qur-aan na Sunnah kwamba ‘dini’ nyengine zote na njia za maisha hazikubaliki Mbele Yake ikiwa mtu huyo anauelewa Uislaam. Qur-aan inaeleza:

 

 وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

 

Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Aal-‘Imraan: 85]

 

Hata hivyo, ingawa Allaah Amefafanua waziwazi kwamba njia nyengine yoyote ya maisha haikubaliwi mbele Yake isipokuwa Uislaam (yaani kunyenyekea Kwake kama inavyofungamana ndani ya Qur-aan na Sunnah), pia Amewaamrisha Waislamu wawe ni wastahamilivu kwa watu wanaojitia kufuata imani nyengine. Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa [Al-Awsat ya At-Tabarani], tunaona kuhusiana na wasio Waislamu waliokuwa wakiishi ndani ya Taifa la Kiislamu:

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Mtu anayeuwa asiye Muislamu chini ya hifadhi (Kiarabu: dhimmi) hatonusa hata harufu ya manukato ya Peponi.”

 

Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya simulizi ya Al-Khaatib, tunaona kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pia alisema:

 

“Yeyote anayemuumiza asiye Muislamu chini ya hifadhi, mimi ni adui wake, na nitakuwa adui wake Siku ya Malipo.”

 

Kwa ufupi, Uislamu hauna ustahamilivu na dhana za uongo, hata hivyo unawastahamilia watu wanaoshikana na dhana hizo. Mfano mmoja wa taariykh ya Waislamu waliokuwa wakiishi katika daraja ya Kiislamu inapatikana kuanzia kipindi cha Spain kwenye hukumu zilizokuwa zikitolewa dhidi ya dini nyengine. Wakati wa maafa yaliyotia fora yaliyokuwa yakifanywa na Wakatoliki wasio waadilifu, baadhi ya Mayahudi wa Spain walihama kwenda Uturuki na hadi leo, kuna jamii ya Wayahudi wanauzungumza lugha ya Spain ndani ya Uturuki.

 

Mfano mwengine unaweza kupatikana wakati wa uvamizi uliofanywa na Vita vya Msalaba Crusader kutoka Ulaya ya Mashariki. Baadhi ya Mabwana wa Kikatoliki wa Ulaya ya Mashariki walifikia hatua ya kubaka, kuua, na kuwateka nyara Mayahudi na Wakristo wenye imani barabara, lakini waliposhinda Waislamu, hao wasiokuwa Waislamu (Mabwana wa Kikatoliki) waliwatumia kama ni nyenzo ya kujiokoa.

 

.../9

 

 

 

 

 

Share