Nani Mwenye Haki Zaidi Kwa Mtoto Wa Kike Baba Au Mume?

SWALI:

 

ASSALAMU ALAYKUM

NANI MWENYE HAKI ZAIDI JUU YA MTOTO WA KIKE AMBAE ASHAOLEWA, BABAKE MSICHANA AMA MUME WAKE MSICHANA, IKITOKEA HITILAFU YOYOTE WAKUSIKIZWA ZAIDI NI YUPI BABA AMA MUME.

 

ALF SHUKRAN KWA WEBSITE JAZAKUMULLAHU KHEYRA WAALAYKUM SALAM

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu masikilizano. Hakika ni kuwa pindi msichana anapoolewa anakuwa ni mke wa mtu, hivyo ruhusa yake na utiifu wake ni lazima iwe kwa mume. Mke huyo hawezi kutoka hata kwenda kwa mzazi wake bila ya ruhusa kutoka kwa mumewe.

 

Bila shaka mume anatakiwa awe ni mwenye kufahamu na kujali maslahi ya wazazi wa mke hivyo asimkataze mkewe kwenda kutazama wazazi wake. Lakini ikiwa amekatazwa kwenda inabidi mke amtii mumewe. Ikiwa kumetokea ugomvi mpaka wanandoa wakaachana basi haki baada ya EDA itakuwa ni baba lakini ikiwa ni ugomvi ambapo mke yuko kwa mumewe haki itakuwa ni ya mume wala sio ya baba.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share