Kusafiri Peke Yake Bila Ya Mahram Na Kusomewa Qur-aan Kwa Muda Mrefu Kwa ajili ya Matibabu?

 

Kusafiri Peke Yake Bila Ya Mahram Na Kusomewa Qur-aan Kwa Muda Mrefu Kwa ajili ya Matibabu?

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Assalam Aleylum. Sheykh ninaumwa na ninataka kwenda nchi ya Kiislamu kusomewa qur'ani. Na sina mahram ninawesa kusafiri peke yangu??? Na mahali napoishe sijapata sheykh wakunisomea natakiwa nisomewe kwa muda mrefu. Assalam Aleykum. [make duua 4 me inshaallah]

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Awali ya yote tunafaa tuelewe kuwa tiba ya Qur-aan ni mwanzo mtu mwenyewe awe ni mwenye kusoma kwani kufanya hivyo kutampatia yeye kinga.

 

Mbali na hilo sijui ni maradhi gani uliyo nayo ambayo tiba yake ni kusomewa Qur-aan? Ingefaa utueleze ugonjwa ili tujue namna ya kukupatia nasiha. Na je, unaishi sehemu gani ambayo haina Mashaykh wa kukusomea wewe Qur-aan? Na je, ni nchi gani hiyo ya ugenini ambayo ungeweza kwenda?

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokataza mwanamke asisafiri bila mahram ni kwa sababu ya zile shida nyingi ambazo anazipata. Nchi ya ugenini ni nchi ya ugeni na hata zile za Kiislamu huenda mwanamke akapata matatizo mengi na hivyo kushindwa kusaidika.

 

Je, umetafuta matibabu aina nyengine kama kwenda kwa madaktari tofauti? Je, katika nchi hiyo hiyo uliyoko hakuna wasomi wa Qur-aan ambao wanaweza kukusomea kiwa unakusudia kusomewa kwa ajili ya Ruqyah?

 

Tukiweza kupata majibu ya hayo tulioyauliza ndio tunaweza kukupatia nasiha ya kwenda au kutokwenda. Kuwa kusafiri kwako huko ni sawa au haifai.

 

Kwa muhtasari ni kuwa safari ya mwanamke bila Mahram haifai hata kwenda Hajj seuze safari nyinginezo.

 

InshaAllaah tuko pamoja nawe kwa du’aa ingawa umetuandikia namba 4 hapo badala ya maneno na hali unauliza jambo muhimu. Kuandika kwa mtindo wa namba si jambo la kistaarabu na pia kunaangusha shakhsiyah ya mtu anayefanya hivyo.

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akukhafifishie maradhi yako na Akufutie madhambi yako kwayo, wewe pamoja na Waislamu wote wenye maradhi na matatizo mbalimbali. Aamiyn.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share