Fajita - (Fa-hee-ta) Ya Kuku (Spanish)

Fajita - (Fa-hee-ta) Ya Kuku  (Spanish)

Vipimo

Kuku kidari (breast chicken) - 2 LB

Mafuta - ¼ kikombe

Mikate ya Tortilla - 12

*Salsa  ya tayari - 1 kikombe

Jibini ya Mozzarella Na Cheddar - 2 vikombe

Masala  ya Taco - 2 vijiko vya supu

Nyanya - 1 kikombe

Saladi - 1 kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kata kata kidari vipande vidogo vidogo uchanganye na masala ya Taco, weka kando.
  2. Kuna (Grate) jibini ikiwa sio ya tayari weka kando.
  3. Katakata nyanya, saladi weka kando.
  4. Weka mafuata katika kikaango (fyring pan), kaanga kuku na masala yake hadi awive, epua.
  5. Panga mikate ya Tortilla katika treya  kisha gawa kuku kila mkate, tia saladi, nyanya.
  6. Nyunyizia salsa ya tayari na jibini iliyokunwa kisha pasha moto kidogo kwa kuweka katika oveni moto wa juu (Grill) kama dakika 5 tu.
  7. Epua na kunja upendavyo, panga katika sahani

*Salsa  ikiwa huna Ya tayari

Vipimo

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Kitunguu - 1

Nyanya - 4

Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya supu

Nanaa iliyokatwakatwa (chopped) - 2 misongo (bunch)

Kotmiri (coriander) iliyokatwakatwa (chopped) - 2 misongo (bunch)

Chumvi - kiasi

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Namna ya Kutayarisha  Na Kupika Salsa

  1. Katakata kitunguu, kaanga katika mafuta.
  2. Tia nyanya zilizosagwa pamoja na nyanya kopo, tia nanaa, kotmiri, chumvi na pilipili.
  3. Kaanga hadi nyanya ziwive na rojo liwe zito iache ipowe.

Kidokezo:

Mikate unaweza kutumia chapatti kavu badala ya Tortillas

Ukipenda ongezea katika mjazo (filling) wake kitunguu na pilipili boga

Masala ikiwa hukupata ya Taco weka masala yoyote upendayo.

 

 

 

Share