Sandwichi Za Soseji

Sandwichi Za Soseji 

 

Mikate Yake:

Soma maelezo katika upishi ufuatao:

Sandwichi Za Mkate Wa Pita Na Nyama

Vipimo

Soseji - 8 -12

Kabeji iliyokatwa nyembamba - 2 vikombe

Karoti - 1

Vitunguu vya kijani - 1 msongo

Slesi za achari ya matango(zilorowekwa katika siki) - (8 -12)

Chumvi - kiasi

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Sosi ya haradali (mustard sauce) - kiasi ya kunyunyuzia

Namna Ya Kutayarisha

  1. Chemsha soseji kiasi unachotaka kufanya sandwichi weka kando.
  2. Katika bakuli, katakata kabeji nyembamba kiasi ifikie vikombe viwili.
  3. Ikune karoti ikatike nyembamba, changanya pamoja katika bakuli.
  4. Katakata vitunguu vya majani, (au kitunguu cha kawaida) tia chumvi, pilipili manga, changanya na slesi za matango.
  5. Fungua mkate kama ilivyo maelezo ujaze mchanganyiko.
  6. Nyunyizia sosi ya haradali (mustard sauce)
  7. Weka soseji juu yake, panga katika sahani zikiwa tayari.

Kidokezo:

  1. Ukipenda  nyunyizia pia kechapu ya nyanya (tomato ketchup) na sosi ya pilipili yoyote upendayo.
  2. Ukipenda pia tia slesi ya jibini (cheese)
Share