Sandwichi Za Mkate Wa Pita Na Nyama

Sandwichi Za Mkate Wa Pita Na Nyama

Vipimo Vya Mkate Wa Pita

Unga wa ngano                                2 mugs

Mafuta                                              2 Vijiko vya supu

Hamira                                              1/2 Kijiko cha chai

Chumvi                                             1/2 Kijiko cha chai

Maji                                                   3/4 mug

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Mikate Ya Pita:

 1. Katika bakuli, changanya unga na vitu vyote.
 2. Kisha kata madonge manane (8).
 3. Sukuma kama chapatti.
 4. Paka siagi na kunja juu yake kama inavyoonekana katika picha.
 5. Kaanga kwenye kikaango (frying pan) huku ukikandamiza na mwiko.
 6. Upande mmoja ukiwiva geuza upande wa pili bila kukunjua katikati.
 7. Epua na itazamishe kwa chini ichuje mafuta- tazama picha:
 8. Ikipoa tayari kutiwa nyama, tuna (samaki), mboga, saladi au chochote upendacho.
 9. Nyama ya Kutia Ndani Yake:
 10. Kausha nyama, kuku kwa thomu, tangawizi chumvi na viungo upendavyo. Unaweza pia kutia tuna na kutia viungo upendavyo
 11. Tia mafuta kidogo tu katika kikaango au sufuria, kaanga vitunguu, thomu, tangawizi, bizari nyembamba ya unga, (cummin), pilipili manga, pilipili ya unga na chumvi.
 12. Kisha tia tomato ketchup kufanya urojo mzito kisha mimina kitoweo chako ulichokausha tia ndimu kiasi.
 13. Ikisha wiva acha ipoe kidogo tayari kutiwa kwenye mikate kama sandwichi.
 14. Namna ya Kutia Kitoweo Kwenye Mikate:
 15. Kunjua mkate, tia urojo kiasi na kitoweo ulichokausha.
 16. Katakata saladi na tia juu yake kama inavyoonekana kwenye picha.
 17. Panga kwenye sahani tayari kuliwa.
 18. Ukipenda unaweza kutia chochote kinginecho

 

 

Share