Mwanamke Ni Lazima Ajifunike Kichwa Akiwa Nyumbani Kwake Au Malaika Hawatoingia Asipofanya Hivyo?

 

Mwanamke Ni Lazima Ajifunike Kichwa Akiwa Nyumbani Kwake Au Malaika Hawatoingia Asipofanya Hivyo?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

A/a/w/wabarakatu.

 

Kwanza Naomba Jina Langu Musilionyeshe Wakati Wa Kunipatia Majibu Kama Majibu Yatapitia Gazetini. Masuala Yangu Ni Mawili

 

Mwanamke Anapokaa Kichwa Wazi Ndani Ya Nyumba Yake Malaika Wema Hawaingii? Hata Kama Yuko Na Maharimu Zake Au Yuko Peke Yake Naomba Ufafanuzi.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Nabiy, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Nabiy. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Swahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.

 

 

Ama kuhusu swali la kwanza hakuna tatizo lolote kwa mwanamke kuwa kichwa wazi akiwa mbele ya maharimu zake kwani hiyo ni sehemu ambayo yaweza kuonekana bila wasiwasi wowote. Allaah Aliyetukuka Anatueleza:

 

..وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ

..wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao,... [An-Nuwr: 31].

 

 

Bila shaka, kichwa ni lazima kifunikwe ikiwa yu mbele ya waume wasio maharimu zake au akitoka nje kwa shughuli zake.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share