Sosi Ya Ukwaju

Sosi Ya Ukwaju

 

Vipimo

Ukwaju - 2 Paketi

Chumvi - kiasi

Tende - ¼ kikombe

Pilipili mbichi - 1

Bizari ya jiyrah (Cummin powder) - ¼ kijiko

Namna ya kutayarisha

  1. Toa kokwa ukwaju, kisha roweka kwenye maji ya moto.
  2. Chambua tende utoe kokwa weka kando.
  3. Tia vitu vyote katika mashine, saga hadi vitu visagike vyote.
  4. Mimina katika bakuli ukiwa tayari kutolewa na aina nyingi ya vyakula upendavyo.

Kidokezo:

  1. Ikiwa huna tenda tumia sukari vijiko 2 viwili vya supu.
  2. Inaweza kuliwa na aina nyingi ya vyakula kama; dehii baree, biriani, nyama/kuku wa kuchoma, mishkaki, sambusa, kachori, katlesi viazi vya duara (chops), kababu na vinginevyo vingi.

 

 

 

 

 

 

Share