Chatine Ya Nyanya Na Kotmiri

Chatine Ya Nyanya Na Kotmiri

Vipimo

Nyanya - 7

Vitunguu - 1

Kotmiri (coriander fresh) - 1 msongo (bunch)

Thomu (kitunguu saumu/garlic) - 7 chembe

Pilipili mbichi ya kijani - 3

Ndimu - 3 kamua

Chumvi - kisia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha nyanya, katakata nyanya na vitunguu mapande uweke katika mashine ya kusagia (blender).
  2. Osha kotimiri vizuri, utoe mizizi, weka katika mashine.
  3. Kamua ndimu, kisha weka vitu vyote katika mashine kisha saga.
  4. Mimina katika kibakuli ikiwa tayari kutolewa kwa wali, na vyakula vinginevyo.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share