Uyoga Unaoota Shambani Na Kuvunwa Ni Sumu?

 

SWALI:

 

Naomba unifahamishe namna ya kutayarisha chakula cha uyoga,na uyoga nilionao mimi ni rangi nyeupe nimeuvuna katika shamba langu,suala langu lipo hapa.

 

1.kwanza uyoga sio sumu?

2.unatayarishwa vipi mpaka upatikane kuwa chakula?

3.Naomba alhidaya inisaidie kwa hayo wenu mwanachama wa alhidaya.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Ama kuhusu Uyoga ni kuwa: kuna uyoga wa kupandwa na uyoga unaojiotea wenyewe bila kupandwa. Uyoga wa kupandwa unatakiwa uwe umepandwa katika sehemu yenye usafi ambayo haitaweza kumuathiri mtumiaji anae taka kuutumia kwa kuula. Muhimu madhali umeuona Uyoga huo upo katika hali ya usafi  basi hauna tabu kuula.

 

Na kuhusu Uyoga unaojiotea hovyo huu haufai kuliwa kwasababu inasemekana unaweza kuwa ni sumu kwani Uyoga wenyewe huo unaojiotea hovyo, Huota sehemu chafu kama katika sehemu za mkusanyiko wa maji maji, Maji yale yanapokuwa yanakaa muda mrefu katika sehemu ile huzaa wadudu na na kufanya utelezi fulani na baada ya muda hutokea huo Uyonga ambao unasemekana ni sumu

 

Ama kuhusu kupikwa kwake ni kwamba kuna aina nyingi za kuutumia uyoga katika mapishi, kwenye michuzi, pasta, au kupika pamoja mboga nyinginezo na vyovyote upendavyo.

 

 

Na Allah Anajua zaidi

 

Share