Kula Tambuu Inafaa?

 

 

Kula Tambuu Inafaa?

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Assalam alaykum
Je kula tambuu inafaa kwa sababu kuna watu waliokuwa wanakula mirungi wamiacha lakini sasa wanakula tambuu

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani ndugu yetu kwa swali lako hilo kuhusu vileo. Hakika tunawapatia pongezi hao ndugu zetu ambao wameweza kuacha mikhadarati mirungi, madawa ya kulevya na pombe na kadhalika. Hii ni ishara kuwa ikiwa mtu anataka kubadilika na kujigeuza katika maovu anaweza kwa tawfiki ya Allaah  (Subhaanahu wa Ta'aalaa), kwani Yeye Anasema:

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ ۗ  

Hakika Allaah Habadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wenyewe wabadilishe yale yaliyomo katika nafsi zao.  [Ar-Ra’d: 11]

 

  

Tufahamu kuwa Uislamu umewka misingi katika mas-ala ya mihadati na mambo mengine ya haraam na halaal. Katika hayo ni kuwa kinacholewesha kwa wingi kidogo pia ni haraam. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anasema:

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Yaliyokuzidieni.” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na  shariy’ah) ili mpate kutafakari. [Al-Baqarah: 219]

 

Kwa hiyo, kuharamishwa kwa ulevi ni kuwa madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa. Hii ni kanuni katika Uislamu, ikiwa kitu kina madhara makubwa huwa hakifai kutumiwa na Muislamu.

 

Hebu tutizame tambuu ina faida gani kwa mwanadamu. Tambuu si lishe yenye kumsaidia mwana Aadam kwa chochote huenda ikawa ina nisba ya vitu kidogo sana kwa manufaa yake. Lakini tizama tambuu hiyo ina vitoeo gani, rangi, tumbaku ya majani yaliyokaushwa, chokaa na vyenginezo. Tumbaku mwanzo ni haram  kwani madhara yake ni makubwa zaidi kwa afya ya mwana Aadam. Ikiwa sigara ambayo imetolewa baadhi ya kemikali inapotengenezwa ina madhara mengi seuze majani yenyewe. Chokaa pia ina madhara na tambuu yenyewe pia ina madhara kwa mwana Aadam anayetumia. Mbali na kuondoa unadhifu kwa kutupa mate ovyo ovyo pindi mtu anapokuwa anakula. Uislamu wenyewe umejengewa na sifa ya unadhifu na usafi.

 

Hivyo, ni vyema mtu asiwe ni mwenye kula tambuu hata ikiwa bila ya vitoeo vyake.

 

Na Allah Anajua zaidi

 

Share