Kaka Ameacha Dada Watatu Shaqiqi, Dada Watatu Na Kaka Kwa Baba

 

SWALI:

 

assalaam alaykum warahmatullaah wa barakatuh

 

Kaka amefariki ana nyumba moja na fedha taslimu huyu kaka ameacha dada watatu baba mmoja mama mmoja na pia ameacha dada watatu pamoja na kaka mmoja ambao wamechangia baba tu. Je hiyo mirathi wanatakiwa wote wapewe? Na kiasi gani kwa kila mmoja?

 

jazaakumullaah khair

 

 

 


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Mirathi iliyoachwa na kaka aliyeaga dunia. Ikiwa limeeleweka vyema swali lako ni kuwa jamaa wa aliyefariki waliobaki ni kama wafuatao:

 

  1. Dada watatu shaqiqi (kwa baba na mama).
  2. Dada watatu kwa baba, na
  3. Kaka kwa baba tu.

 

Kulingana na swali hilo inaonyesha aliyefariki hakuacha wazazi, mke wala watoto. Ikiwa hivyo ndivyo, basi urithi wa jamaa wa aliyefariki ni kama katika jedwali ifuatayo:

 

 

Namba

Uhusiano na Aliyefariki

Mgao

1

Dada Shaqiqi 1

2/9 (22.222)

2

Dada Shaqiqi 2

2/9 (22.222)

3

Dada Shaqiqi 3

2/9 (22.222)

4

Dada kwa Baba 1

1/15 (6.667)

5

Dada kwa Baba 2

1/15 (6.667)

6

Dada kwa Baba 3

1/15 (6.667)

7

Kaka kwa Baba

2/15 (13.333)

 

JUMLA

1 (100)

 

Kwa vitu vilivyobaki vya kurithiwa ni nyumba na fedha taslimu alizoacha aliyefariki. Fedha taslimu zitagawanywa kulingana na mgao ulio hapo juu, ama nyumba itategemea wanavyoona warithi. Inaweza kupangishwa, na ijara inayopatikana igaiwe kwa mgao kila mmoja haki yake, au inaweza kuuzwa na pesa kupatiwa kila mmoja anachostahiki au mwenye uwezo akainunua miongoni mwa ndugu kisha hizo fedha zilizopatikana kwa njia hiyo kuweza kugawia kila mmoja anachostahiki.

 

Ikiwa ni nyumba kubwa ambayo inaweza kugawia kila mmoja bila matatizo na kila mmoja akapata haki yake anayostahiki kutakuwa hakuna matatizo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share