Mume Ameoa Bila Cheti Cha Ndoa Amefariki Je, Mke Anaweza Kumrithi?

 

SWALI:

 

Assalmu alaikum

Shukran sana kwa majibu ya maswali yangu. Allah awajaze na kila la kheri. Nataka ongeza mume ameowa mke akaishi nae na mpaka akafariki. Lakini hana cheti cha kuwa ameowa je anaweza kurithishwa. Shukran.


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mke kuolewa mpaka mumewe kuaga dunia bila ya cheti cha ndoa.

 

Tufahamu kuwa cheti si katika masharti katika kusihi ndoa kishari’ah baina ya Waislamu. Ndoa katika Uislamu ina masharti yake kama kuwepo walii, mashahidi wawili, mahari, kuridhika mume na mke, na lau hayo yametimia basi ndoa hiyo ni sahihi. Na ikiwa ndoa ni sahihi mume au mke anapoaga mwanzo kila mmoja ataweza kumrithi mwenziwe.

 

Kwa hiyo, mke huyo atakuwa ni mwenye kumrithi mumewe aliyeaga dunia bila haja ya kuwepo cheti.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share