Mkate Wa Mofa (Yemen)

Mkate Wa Mofa  (Yemen)

 

 

Vipimo

 

Unga wa mahindi - 1 mug

 

Unga wa mtama - 2 mugs

 

Kitunguu maji - 1 kikubwa

 

Chumvi - 1 kijiko cha chai

 

Sukari - 1 kijiko cha chakula

 

Hamira - 1 kijiko cha chai

 

Maji -  3 mugs

 

Namna Ya Kutayarisha Na  Kupika

  1. Upike unga wa mahindi kama uji kwa dakika kama tano   na maji mug mbili.   
  2. Uache upoe tia unga wa mtama na vitu vyote vilivyobaki pamoja na ile mug moja ya maji iliyobaki.
  3. Uache mpaka uumuke.
  4. Fanya maduara duara halafu tandaza uchome kwa moto mdogo kama chapati bila ya mafuta kwenye kikaango (frying pan). Choma mmoja mmoja yote hadi umalize..
  5. Iipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa na mchuzi wa nazi wa samaki au kuku au vyovyote upendavyo.
Share