Du'aa: Kuna Du’aa Ya Kunuia Kwa Ajili Ya ‘Iyd

 

Kuna Du’aa Ya Kunuia Kwa Ajili Ya ‘Iyd

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

asalamu aleikum ndugu zetu al hidaaya tunashukuru sana kuwa mafunzo yenu hapa tulipo tunafayidka sana na nyi mungu awabariki awazishie hima ya kufunza ulimwengu kulingana na dini yetu ya haki

basi ndugu naomba mutufune jinsi ya kunuwia idul fitri basi munielze dua yake ndugu zangu kwa haya machche shukran

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu Swalaah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hatukupata mafunzo yoyote  yaliyo Swahiyh kuhusu kutia nia kwa ajili ya Sikukuu ya  'Iydul-Fitwr wala 'Iydul-adhwhaa na wala hakuna du'aa khaswa iliyothibiti katika mafunzo ya dini yetu.

Ikiwa umekusudia kutia nia kwa ajili ya Swalah ya 'Iyd basi hilo ni kama kawaida ya kutia nia katika ibaada yoyote nyengine, nayo ni kuweka moyoni pekee na sio kuitamka.  

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

 

Vipi Kutia Niya Ya Ibaada?

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share