Iyd: Kunyanyua Mikono Katika Kila Takbiyrah Ya Ziada Kwenye Swalaah Ya 'Iyd Ni Sahihi?

 

 

Kunyanyua Mikono Katika Kila Takbiyrah Ya Ziada Kwenye Swalaah Ya 'Iyd Ni Sahihi?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Assalam Aleyqum,
 
Je baada ya kufunga swala  katika swala IDD unapo piga TAKBIRA je unainua mikono kama unafunga swala au unapiga takbira wakati mikono ikiwa umeifunga kifuani kama kawaida ?

 

 

 

JIBU:

 

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Suala la kunyanyua mikono kwenye Swalaah ya 'Iyd katika Takbira za ziada halijathabiti kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bali limefanywa na Swahaba kama Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma). Na ndio 'Ulamaa wakasema kutokunyanyua mikono ndio sahihi zaidi kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakufanya hivyo. Lakini pia wamesema ikiwa mtu atanyanyua mikono hakuna tatizo kwani baadhi ya Swahaba walifanya hivyo.
 

Kwa hiyo, utakapokuwa unaswali Swalaah ya 'Iyd, utanyanyua mikono yako katika kufunga Swalaah wakati wa Takbiyratul Ihraam, kisha baada ya hapo utaiacha mikono yako kifuani bila kuinyanyua wakati unapopiga hizo Takbiyrah saba za ziada katika rakaa ya kwanza na zile tano katika rakaa ya pili.
 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share