Swalaah Ya jamaa Inafaa Nyumbani?

SWALI: 

assalaam aleykoum warahmatullahi wabarakaatu, ama baada ya salaam napenda kuuliza suala langu ambalo limekuwa linanitatiza kwa muda mrefu nalo nikwamba:- jee kwa mfano mimi naishi mbali na msikiti, inafaa kuswali jamaa nyumbani kwangu na mke wangu na watoto wangu, ambao watoto ni mchanganyiko wa kiume na kike, na kama inafaa jee tuupange vipi mstari wa maamuma, na jee tutapata fadhila za jamaa? Nitashukuru saana kama nitajibiwa suala hili kupitia e-meil yangu ambayo ni 

ahsante sana, samahani penye kosa.

 


 

JIBU:

Shukrani kwa kaka yetu ambaye ameuliza swali hili kuhusu Swalah ya Jamaa nyumbani.

Ifahamike kuwa Swalah inayopendeza kwa Allah na yenye thawabu nyingi ni ile inayoswaliwa Msikitini kwa wanaume.

Zipo Hadithi nyingi zinazoelezea thawabu ya Swalah ya jamaa. Moja ni ile ya Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa amesema: “Swalah ya jamaa ina thawabu 27 zaidi kuliko Swalah ya mtu peke yake” [Al-Bukhari na Muslim].

Na pia ipo riwaya ya daraja 25 na nyengine kuanzia 23 mpaka 29.

Lakini ikiwa kuna udhuru unaokubalika kisheria ya kutoweza kuswali Swalah kwa jamaa Msikitini basi mutaswali jamaa nyumbani pamoja na kina mama na watoto. Na maana ya jamaa ni kuwa munaswali pamoja na watu wasiopungua 2. Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amehimiza hata watu wakiwa katika jangwa na ni zaidi ya wawili basi waswali kwa jamaa na ikiwa hawatafanya hivyo basi shetani ametawala (Abu Dawud kwa Isnadi iliyo Hasan).

Hivyo, mukiswali jamaa thawabu munazopata zitakuwa ni sawa kukiwa na udhuru kama ulivyoelezea.

Katika jamaa hiyo, mwanaume ndiye ataswalisha na kukiwa na wanaume wengine watasimama nyuma yake, watoto wa kiume nyuma yao na kina mama watakuwa mwisho baada ya laini ya watoto.

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share