Ufafanuzi Wa Shemeji Yake Aliyefariki Anamjia Ndotoni Kuwa Kuna Mtu Anamfanyia Uchawi – Je Aende Kwa Maalim Atolewe Uchawi?

 

 

Ufafanuzi Wa Shemeji Yake Aliyefariki Anamjia

Ndotoni Kuwa Kuna Mtu Anamfanyia Uchawi –

Je Aende Kwa Maalim Atolewe Uchawi?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI

 

Assalam Alaykum Wa Rahmatulahi Wabarakatu

 
Suali:
 
Nakushukuruni kwa jibu lenu na sasa nitakuambia kwa kirefu labda utanifahamu.
 
Nina mtoto wa dada yangu wa kike school zilipofungwa jamaa wa baba yake wakaja kumchukuwa akiwa ana miaka 7 hata bado hajabalegh, na akaaa muda wa siku kumi katika hizo siku kumi mama mwenye nyumba akamwambia lazima alale nae chumbani kwake aweke godoro chini ikiwa huyo mama ana watoto wa kike wana chumba chao.

 
Siku ya kwanza - ilipofika saa 12 za usiku yule mama akavuwa nguo zote akaenda kumchutamia yule mtoto wa dada yangu, yule mtoto alikuwa macho akamwambia bibi unafanya nini - yule bibi akakimbilia chooni yule mtoto wa dada yangu akaanza kuingiwa na khofu lakini kaogopa kuwaambia watoto wa yule mama.

 
Siku ya pili - Ilipo fika saa 2 za usiku yule mama akaona kuwa yule mtoto ameshalala akafungua kabati lake akatoa sahani nyeupe akawa anasema nayo - je mnamtaka huyu mtoto ikajibu sauti nzito sana ndio tunamtaka akawaambia njooni mumchukuwe kabla ya sala ya alfajir wakasema haya - basi yule mtoto akamuuliza bibi unasema na nani yule bibi kwa kustuka ile sahani ikamponyoka na kuvunjika - yule bibi akamjibu kuwa mfanyakazi ameweka sahani ndani ya kabati lake hajui kwa nini.

 
Siku ya tatu - Ilipofika usiku anataka kwenda kulala yule bibi akatoa ndizi akamlazimisha lazima aile yule mtoto akasema mimi sipendi ndizi akamwambia lazima ule akatokea mjukuu wake akamwambia mimi napenda ndizi nitaila mimi yule bibi akaruka na kumnyanganya mjukuu wake ile ndizi na kumpa yule mtoto wa dada yangu lazima aile "akaila".

 
Ilipofika siku ya nne yule mtoto wa dada yangu akaanza kulia kuwa anamtaka mama yake akamwambia nikusikie tena unasema unataka kwenda kwenu utaniona.

 
Siku ya tano - yule mtoto wa dada yangu ilipofika saa 12 za usiku amaamua kutoroka lakini sehemu waliokuwa wakikaa ni mitende na visima hakuna hata nyumba ya jirani "akatoka mpaka nje akaogopa na kurudi ndani akasema leo sitaki kulala kwenye chumba chako nataka kulala na wenzangu yule bibi akamkatalia mpaka watoto wa yule bibi wakubwa walikuwa kwenye miaka 25 - 30 wakamuuliza mama yao mama kwa nini huyu mtoto anakuogopa ikiwa huyu mtoto anatupenda sana na akija kwetu hataki kurudi kwao.

 
Basi mambo yakaendelea kwa siku kumi. Ikiwa siku kumi hizo sisi sote tulikuwa tunashughulika na ndugu yake aliyekuwa kwenye ICU ana maradhi ya damu SICKLE CELLS.

 
Baada ya siku kumi yule mtoto akarudi nyumbani hajamwambia mtu yeyote kama alikuwa anafanyiwa mambo. Siku moja niliamua kuwachukuwa watoto wa ndugu zangu wote kuwapeleka Garden tulipo fika Garden Yule Mtoto wa kike alikuwa ana miaka 7 akavua nguo zote na kwenda mbio nilikuwa na Allaah Tu sina mtu wa kunisaidia nikampigia kaka yangu simu nikamueleza akasema njoo nyumbani kwani ndio karibu nikaweka cassete ya Qur-aan na wote kwenye gari tukawa tunasoma Qur-aan tulipofika kwa kaka yangu ilikuwa adhana ya Maghrib kaka yangu akasema direct aende kutawadha na kuja kusali alipokuwa kwenye msala na kaka yangu basi wote wawili wakasukumizwa mpaka wakaanguka na aisikiyapo adhana basi yeye ndio wazimu unazidi.

 
Tukaanza kumtibia kwenye hospital ya vichaa lakini result zikaja ok hana matatizo ya hospital waka huwa mtoto akaanzwa kufungwa na kamba kwenye chumba ikiwa huyo mtoto amezaliwa africa lakini amekuja Oman akiwa na miaka miwili na nusu na wakati huwo hajui lugha nyingine ila arabic na school daima anatokea mtu wa kwanza tu.

 
Ikaenda zaidi ya miaka miwili ikiwa mama yetu alifanya Umra Na Hajj hataki kwenda kwa maalim lakini ilipokika siku yeye mwenyewe akaamua kukubali kwenda kwa maalim mtoto alitumia dawa kwa maalim tofauti kwa muda wa miaka mitatu kisha tukapata maalim mmoja yeye akasema mimi sina tiba ile tumuombe Allaah Subhanahu wa Ta'aalaa Yeye Ndie Kila Kitu. Basi akamuandikia kombe yule mtoto baada ya kunywa kwa muda wa siku saba akamwita dada yangu mwingine na kumuhadithia yote aliyekuwa alifanyiwa kwa muda wa siku kumi na yule bibi.

 
Mtoto huyo ametibiwa tangu ana miaka saba mpaka sasa ana miaka 20 na sisi tulikuwa tunampenda sana huyo bibi aliyefanyia mambo huyo mtoto hatujafikiria kwenye maisha yetu kama anaweza kufanya hivyo. Je huyo si mchawi? Na yote aliyeyafanya ni uislam kumuharibu mtoto wa mwenzako? Je mambo kama hayo je hutokwenda kwa maalim ikiwa yeye ni binaadam kama wewe na anmuomba Allaah Subhanahu wa Ta'aalaa Kwenye Dawa Zake?

 
SASA hivi mtoto ana miaka 20 na ametibiwa alhamdulilah tunamshukuru Allaah Subhanahu wa Ta'aalaa kwa kututakabalia maombi na dawa za huyo maalim lakini bado hayuko sawa je Tufanye Nini ikiwa hata kwa sheikh Khalil (Mufti wa Oman) tumekwenda tumepewa makombe na cassete lakini mambo bado sasa nahitaji msaada wenu.

 

Assalam Alam Alaikum

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu yaliyomkumba mtoto wa dada yako. Hakika kulingana na kisa chake kwa hayo aliyofanyiwa binti huyo ni kama uchawi aliofanyiwa na mama huyo. Kwa hakika ni kuwa kufanya hivyo kwa mtoto wa mwenzako ni dhuluma kubwa na Uislamu umekuja kuondosha dhuluma aina zote. Mwisho wa mwenye kudhulumu si mzuri hapa duniani na Kesho Aakhirah. Na kwa ule uzuri wa Uislamu ambao tumeelezewa ni kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa mpendelee mwenzio unavyopendelea nafsi yako.

 

Hilo alilofanya huyo bibi ni makosa Kiislamu kumfanyia Muislamu na hata asiyekuwa Muislamu. Hata hivyo, jambo hilo lishafanyika sasa ni sisi kutazama njia ya kuweza kumtibu na kumsaidia kijana ambaye sasa ni tayari amebaleghe. Njia za kutafuta matibabu ni lazima ziende sambamba na sheria ya Kiislamu bila kuingia katika njia za utata wala shirki kwani hizo ni amali katika madhambi makubwa yaliyokatazwa na sheria. Hayo aliyofanyiwa mtoto wenu inaonekana kwa uwazi kuwa ni sihri, na haifai kuundosha uchawi kwa kutumia uchawi. Hivyo, ni lazima turudi katika Dini na kufuata njia sahihi za kufanya shughuli hiyo. Katika njia bora na sawa ni kuweza kumfanya na kumfundisha msihiriwa mwenyewe awe ni mwenye kusoma zile Suwrah, Aayah na Adhkaar ambazo ni kinga kwa Muislamu. Na njia nyepesi ni kupata kijitabu ambacho kinaitwa Hiswn al-Muslim.

 

Njia nyingine ni kumpeleka mgonjwa kwa Shaykh wa Sunnah ambaye anaweza kumsomea Suwrah, Aayah na Adhkaar za kisheria (za Ruqyah) na kuweza kutoa hiyo sihri kama ipo. Mas-ala ya kwenda kwa waalimu ambao mara nyingi wanatumia mbinu zisizoeleweka au uchawi wenyewe, ni mas-ala yasiyofaa kabisa kisheria katika Dini yetu.

 

Tunamuombea Allaah Aliyetukuka Ampe ponyo ya haraka na atoke katika balaa hiyo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share