Anapoweweseka Usiku Asomewe Surah Gani?

 

Anapoweweseka Usiku Asomewe Surah Gani?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalam aleykum 

Hivyo naomba nikuulize. Katika hili jibu lako kuhusu  Rukya, nime ona ume gusia kusoma Al- Baqarah. Lakini mimi sija jua kwa nini hasa una soma Al-Baqarah. Mfano hai, mimi juzi nilikuwa najiandaa kulala na mara mke wangu akaanza kuweweseka na kisha kuanza kulia na sauti ikiwa ya taabu kutoka. Lakini baadae ilikuja sauti ambayo sio yake na ikitoka kinywani mwake na kuni ambia nimsomee Alif lam mim , Dukhan na dua yoyote. Mara baada ya kufanya hivyo basi alirejea katika hali yake ya kawaida. Kitu alicho nieleza ni kuwa alikuwa ana ona mtu mbaya. Jee una weza kunielewesha mambo haya na kwanini sura hiyo. Maanake sio ndogo lakini ilinibidi niisome yote hapo juzi kama saa nne na nusu usiku.

Nita shukuru kwa jibu lako au hata kama utapata msaada kutoka kwa yoyote alie mjuzi zaidi kuni fafanulia hayo.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Suwrah Al-Baqarah imegusiwa kuwa ni miongoni mwa Suwrah za Ruqyah khaswa Ayaatul-Kursiy na Aayah mbili za mwisho, kwa vile mwenye kusoma huwa ni kinga ya shaytwaan kuingia katika nyumba. Dalili ni:  

عن ‏ ‏أبي هريرة ‏ رضي الله عنه ‏أن رسول الله ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏قال‏ : ((لا تجعلوا بيوتكم مقابر إن الشيطان ينفر من البيت الذي تقرأ فيه سورة ‏ ‏البقرة))    

Kutoka kwa Abu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba  Nabiy (Swallah Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msifanye nyumba zenu makaburi, hakika Shaytwaan anakimbia nyumba ambayo inasomwa Suwrah Al-Baqarah" [Muslim]   

عن ‏ ‏أبي مسعود ‏ ‏رضي الله عنه ‏ ‏قال :‏ ‏قال النبي‏ ‏صلى الله عليه وسلم((  من قرأ بالآيتين من ‏ آخر سورة ‏ ‏البقرة ‏ ‏في ليلة كفتاه )) [ رواه البخاري   .

Kutoka kwa Abu Mas’uud (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swallah Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakayesoma Aayah mbili mwisho wa Suwrah Al-Baqarah usiku zitamtosheleza" [Al-Bukhaariy]  

عن النعمان بن بشير عن النبي صلى الله عليه وسلم قال : (( إن الله كتب كتاباً قبل أن يخلق السماوات والأرض بألفي عام أنزل منه آيتين ختم بهما سورة البقرة، ولا يقرآن في دار ثلاث ليال فيقربها شيطان)) [ رواه الترمذي وصححه الألباني في صحيح الجامع الصغير  

Kutoka kwa an-Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba  Nabiy (Swallah Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: "Hakika Allaah Ameandika Kitabu kabla ya kuumba mbingu na ardhi kwa muda wa miaka eflu, Akateremsha Aayah mbili alizozimalizia Suwrah Al-Baqarah, na wala hazisomwi katika nyumba siku tatu akakaribia Shaytwaan" [At-Tirmidhiy na kaisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Al-Jaami’us-Saghiyr]

 

Mwenye kukumbwa na majini, uchawi, hasad au shari yoyote hivyo inampasa ashikilie kusoma Suwrah hii tukufu iwe ni tiba kwake au vile vile isomwe hata na asiyekumbwa iwe ni kinga kwake.

 

Ama kuhusu hali ya mke wako hiyo kutokwa sauti ya mtu mwingine na kutaka kusomewa Suwrah Al-Dukhaan, ni kwamba hakuna dalili yoyote inayothibiti kuwa Suwrah hiyo ni tiba au kinga ya Shaytwaan. Kwa ujumla Qur-aan yote ni tiba na kinga, hivyo huenda ikawa ndio sababu ya kutulia hali yake aliposomewa maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

Yafutayo atekeleze mwenye kutaka kujikinga au kujitibu na kukumbwa na shari yoyote:

 

Kwanza: Kusoma Qur-aan kwa wingi na khaswa Suwrah Al-Baqarah kila baada ya siku tatu kwa mfululizo hadi apeukane na shari iliyomkumba.

  

Pili:  Kusoma Aayah Zote Tulizonukuu Katika Jibu Hilo La:

 

Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

 

Tatu:  Kusoma Adhkhaar Za Asubuhi Na Jioni:

 

Nne: Wakati wa kulala; kabla na akishtuka usingizini kwa kuweweseka au kwa njozi mbaya, basi asome  Adkhaaar za asubuhi na jioni zilizomo katika Kitabu cha Hiswnul Muslim kilichoko Alhidaaya pamoja na du’aa nyingine zilioko katika viungo vifuatavyo kuwakimbiza viumbe viovu usiku na mchana.

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

 

027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

 

028-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Kulala

 

029-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unapojigeuzageuza Usingizini Usiku

 

030-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Wasiwasi Usingizini Au Kusikia Uoga Na Mfadhaiko

 

031-Hiswnul-Muslim: Ipasavyo Kufanya Na Kusema Mwenye Kuota Ndoto Njema Au Mbaya

 

 

Tano: Anapoingia mtu nyumbani kwake atoe salamu na aseme:

((بِسْـمِ اللهِ وَلَجْنـا، وَبِسْـمِ اللهِ خَـرَجْنـاَ، وَعَلـى رَبِّنـا تَوَكّلْـناَ))

BismiLLaahi waljanaa wa BismiLLaahi kharajnaa wa 'alaa Rabbinaa tawakkalnaa.

((Kwa jina la Allaah, tunaingia, na kwa jina la Allaah tunatoka, na Rabb wetu tunamtegemea))

 

Hii ni kutokana na dalili:

 

عن جابر بن عبد الله أنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقول : (( إِذَا دَخَلَ الرَّجُلُ بَيتَهٌ فَذَكَرَ اللهَ عِندَ دُخُولِهِ وَعِندَ طَعَامِهِ ، قَالَ الشََّيطَانُ : لَا مَبِيتَ لَكُم وَلَا عَشَاءَ ، وَإِذَا دَخَلَ فَلَم يَذكُرِ اللهَ عِندَ دُخُولِهِ ، قَالَ الشَّيطَانُ : أَدرَكتُمُ المَبِيتَ ، وَإِذَا لَم يَذكُرِ اللهَ عِندَ طَعَامِهِ قَالَ : أَدرَكتُمُ المَبِيتَ وَالعَشَاءَ )) رواه مسلم

Imetoka kwa Jaabir bin 'Abdillaahi kwamba kamsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Anapoingia mtu nyumbani kwake au anapokula akamtaja Allaah, Shaytwaan husema (akijiambia mwenyewe):  'Huna mahali pa kukaa wala chakula'. Lakini akiingia bila ya kumtaja Allaah, Shaytwaan husema (akijiambia mwenyewe): 'Umepata mahali pa kukaa'. Na asipomtaja Allaah wakati wa kula, husema (akijiambia mwenyewe):  Umepata mahali pa kukaa na kula" [Muslim]

 

Sita: Kujiweka Katika Hali Ya Twahara

 

Inavyojulikana kwamba wanawake zaidi ndio wanaokumbwa na majini. Na sababu mojawapo kuu ambayo wengi ima  wameghafilika nayo, au sio wengi wanaoitambua kwamba ni kutokana na kutokujiweka katika tohara kiukamilifu. Upelelezi wa baadhi ya ’ulaama wetu wameona kwamba ni kutokana na mwanamke kutokujisafisha vizuri kwa maji katika sehemu zake za siri anapomaliza haja yake msalani. Khaswa mkojo na mirusho yake inayobakia sehemu hizo.  Mkojo wa mwanamke najsi yake ni tofauti na ya mwanamume. Kwa hiyo mwanamke awe anahakikisha kuwa anajisafisha vizuri sana ili aondoshe najsi ya mkojo na aweze kujiepusha na kukumbwa na viumbe hivyo.

 

Maelezo zaidi kwa upana yanapatikana katika kiungo kifuatacho:

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share