Anaota Ndoto Mbaya, Anatishwa, Amefukuzwa Kazi, Je, Majini Wamemkumba?

 

 

Anaota Ndoto Mbaya, Anatishwa, Amefukuzwa

Kazi, Je, Majini Wamemkumba?

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Assaalam alekum. Naomba kusaidiwa haya majini mahaba kweli yako na dawa yake ni nini? Ifi yangu anasumbuliwa sana na hayo majini inamfanya hata kaka yangu kumdhuru kwani anapokuwa nae na yeye anapata ndoto zakutishiwa kuuliwa na afunguapo macho anaona vitu vya kutisha na hata kazi aliokua nayo kafukuzwa kifupi maisha yake yamebadilika sana na kuwa mabaya. Hatujui tufanye nini? Tunaomba mtusaidie. In shaa Allaah

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hili ni suala ambalo ni sahali sana. Awali ya yote inatakiwa katika nyumba anayoishi aliyekumbwa na hayo kusomwa Qur-aan na ni bora zaidi ikiwa muathiriwa atasoma mwenyewe. Na hasa kabisa nyumba inayosomwa Suwratul-Baqarah hakuingii Shaytwan kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

عَنْ سَهْل بْن سَعْد قَالَ قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((إِنَّ لِكُلِّ شَيْء سَنَامًا وَإِنَّ سَنَام الْقُرْآن سُورَة الْبَقَرَة وَمَنْ قَرَأَهَا فِي بَيْته لَيْلًا لَمْ يَدْخُل الشَّيْطَان بَيْته ثَلَاث لَيَالٍ وَمَنْ قَرَأَهَا نَهَارًا لَمْ يَدْخُل الشَّيْطَان بَيْته ثَلَاثَة أَيَّام)) القاسم الطبراني وأبو حاتموابن حبان في صحيحه، وابن مردويه

Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila kitu kina kipeo cha kudhibiti (na kuangaza yaliyo chini) na Al-Baqarah ndio kipeo cha Qur-aan. Atakayesoma Al-Baqarah usiku nyumbani kwake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba yake nyusiku tatu. Na atakayesoma mchana ndani ya nyumba yake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu.” [Atw-Twabaraaniy (6/163), Ibn Hibbaan (2/78) na Ibn Mardawayh, Swahiyh At-Targhiyb (2/314)]

 

Pili, anaweza kujifanyia  Ruqyah ya ki Shariy’ah isiyokuwa na ushirikina.  

Na maudhui ya Ruqyah na Suwrah au Aayah zinazopaswa kusomwa zinapatikana katika viungo vifuatavyo:

 

 

Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Du’aa Za Ruqyah (Kinga) Faida Na Sharh Zake

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share