Baba Anaamrishwa Usingizini Aingie Katika Shirki – Alipokataa Kapata Maradhi Ya Kupooza. Je, Ni Ndoto Au Ni Wanga Washirikina

SWALI:

 

Asalamu alaykum, Waislamu wenzangu. Napenda kuuliza suala. Baba yangu ana matatizo, kwa kawaida huwa anaota anaendewa na watu [ndugu zake] usingizini na anaambiwa [tunakutaka uingie kwenye chama chetu za uchawi] Baba alijibu siwezi, akaendewa tena akaambiwa kama hukutupa kauli ya ndio basi tutakalofanya tunajua wenyewe na tutakutia adabu akasema nitieni, lakini hatowezekana. Basi akapata maradhi ya baridi [yakupooza]. Akaendewa tena [usingizini] akaambiwa jee unaona adabu tuliyokutia, akawajibu nimeona lakini katu sitoingia kwenye chama chenu katu. Je mashekhe kweli hii inawezekana au ni ndoto za sheytwani tu na kama inawezekana naomba tiba ya kufanya. Kwa sababu kuna groupu inaplani kwenda kwa waganga. Naomba majibu haraka. AHSANTENI.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu ndoto anazoota babako usingizini.

 

Hayo uliyoyaeleza ni katika ishara miongoni mwa ishara za uchawi unaofanywa na watu wenye nia mbaya kwa mtu fulani.

 

Suala la baba yako ni sahali sana na wala haina utata wa aina yoyote. Kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kumpata Shaykh mcha Mungu aliye mtaalamu katika kumsomea mgonjwa kisomo cha sheria bila kutumia mazingaombwe wala uchawi. Ikiwa kweli amefanyiwa uchawi basi ishara hizo zitaonekana na ataweza kutibiwa. Na ikiwa mwenye bado anaweza kusoma basi awe anasoma zenye Aayah za kinga kama Aayatul Kursiy, Aayah mbili za mwisho za Suratul Baqarah, Suratul Ikhlaasw (mara 3), al-Falaq na an-Naas (mara tatu tatu). Pia awe ni mwenye kusoma Adhkaar za asubuhi na jioni kwa kutumia kijitabu Hiswn al-Muslim kinachopatikana hapa Hiswnul Muslim.

 

Maelezo zaidi kuhusu Surah Na Aayah Za Ruqya, bonyeza katika viungo vifuatavyo:

 

Naingiliwa Na Majini

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Anapoweweseka Usiku Asomewe Surah Gani?

 

Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

 

Nimeambiwa Nina Jini La Kiislamu Kwa Sababu Ya Kupenda Sana Dini

 

Na hatuna shaka kuwa atapona kwa kutumia kisomo hicho. Tunawaombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kila la kheri.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share