Mwanaume Kuvaa Fedha Inajuzu?

 

Mwanaume Kuvaa Fedha Inajuzu?

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

 

Assalaam alaykum warahmatullah wabarakaatuh.

Allah subhaanahu wa Taala akujazeni kheri kwa kazi mnayoifanya. amin Naomba kuuliza je nijuavyo ni haramu kwa m/mme kuvaa dhahabu, je ni halali kuvaa fedha?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Bila shaka kama ulivyosema kuwa dhahabu haifai kuvaliwa na mwanamme, nayo ni halali kwa mwanamke tu.

 

Ama fedha inaruhusiwa kwa mwanamme na mwanamke, lakini kwa mwanamme ni kuivaa kwenye kidole (yaani pete) au kwenye mkono (yaani saa). Hadiyth ifuatayo ni dalili ya kukubalika fedha kwa mwanamume.

 

Amesimulia Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa pete ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ya fedha yenye kijiwe cha Habasha ndani yake [Muslim].

 

Ama kuvaa fedha kama bangili, au kipuli, au mkufu ambayo ni mapambo ya kike haifai kabisa kwa mwanamme.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share