Kiwango Gani Mke Avumilie Maudhi Ya Mume? Na Sababu Zipi Za Kuomba Talaka?

 

SWALI:

 

Nawapongeza kwa website nzuri kama hii ambayo inawafungua kili na macho ya Waislam kwa jumla.  Pili Mngu awabariki na awape kila la kheri duniyani na Akhera nyinyi na jamii Muslimeen.

 

Suali langu ni Hadi kiwango gani mke anaruhusiwa kuchukua maudhi ya mume? Au kuliulizia vengine sababu gani zina mpa mke haki ya kudai talaka? Wasalaam Warahmatullahi wa barakatu hu. Jazakah Allah Kher.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu kiwango cha mke ambacho anaweza kumvumilia mumewe.

Uislamu hakika haukuweka kiwango maalumu isipokuwa katika matatizo hayo mke anatakiwa afanye kila njia ya kuweza kuihifadhi ndoa yake. Hata hivyo, inategemea pia na makosa ya mume anayofanya. Kwa mfano, ikiwa mume haswali, ni mlevi au hatekelezi baadhi ya ‘Ibaadah za Kiislamu inatakiwa uvumilivu uwe ni mdogo kwani hakuna faida yoyote ya kukaa na mume kama huyo.

 

Uvumilivu wa kiwango cha mwisho ni kutazama vipengele na kutekeleza mambo yafuatayo:

 

  1. Kuzungumza naye ana kwa ana kwa njia nzuri ili aweze kujirekebisha mienendo na matendo yake.
  2. Ikiwa hakujirekebisha, basi itisha kikao baina yako, na yeye, wawakilishi wako (kama wazazi au walezi) na wawakilishi wake.
  3. Ikiwa haikufaulu, basi itabidi hiyo kesi yako uipeleke kwa Qaadhi ikiwa yupo, au Shaykh mwenye kuaminika kwa uadilifu na usome na hapo hatuna shaka ufumbuzi utapatikana.

 

Tunakutamania upate suluhisho la karibu kuhusu matatizo yako inshaAllaah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share