Makaroni Ya Kuku Na Mboga Mchanganyiko

Makaroni Ya Kuku Na Mboga Mchanganyiko

 

 

Vipimo

 

Makaroni ya aina yoyote - 375 gms

Nyama ya kuku iliokatwa vipande - 1 Lb

Kitunguu - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 Kijiko cha supu

Mdalasini - ¼ Kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Pilipili manga ya unga - ¼ Kijiko cha chai

Ndimu - ½

Kidonge cha supu - 1 Kidonge

Mboga za barafu (frozen vegetable) - 2 Vikombe vya chai

Namna Ya kutayarisha na Kupika

  1. Katika sufuria, mtie kuku, chumvi, pilipili manga, thomu na tangawizi, kitunguu, mdalasini na kidonge cha supu.
  2. Weka katika moto na mpike hadi awive.
  3. Kisha utoe mifupa na uchambue nyama ndogo ndogo weka kando.
  4. Chemsha makaroni kwa chumvi na mafuta kidogo kwa kufuata maagizo yake katika pakiti.
  5. Karibu na kuiva tia (frozen vegetable) mboga za barafu na ziache dakika moja hivi.
  6. Ikishaiva mwaga maji kwa kuchuja na weka katika sufuria.
  7. Changanya na kuku uliomtayarisha na kamulia ndimu na itakuwa tayari kwa kuliwa na kechapu ya nyanya (tomato ketchup).

Kidokezo:

Unaweza katakata vipande vidogo dogo freshi vya keroti, maharage machanga mabichi ya maganda na njegere kama huna (frozen Vegetable) 

 

Share