Spageti Na Sosi Ya Nyama Ng'ombe Vipande

Spageti Na Sosi Ya Nyama Ng'ombe Vipande

Vipimo

Spaghetti - 500g

Maji - 1lita na nusu

Chumvi - 1 kijiko cha supu

Tomato ya kopo - 3 Vijiko vya supu

Tomato (fresh) - 3

Kitunguu maji - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Nyama  bila mifupa - nusu kilo

Tangawizi mbichi ilyosagwa - 1 kijiko cha supu

Mafuta - nusu kikombe cha chai

Namna ya kutayarisha sosi

  1. Nyama ikoshe na ukata vipande (size) upendayo,tia sufuriani.
  2. Itie tangawizi,chumvi nusu, na ipike kwa kuikausha moto wa chini bila kuongeza chochote paka itoe maji na kutowa harufu ya supu zima jiko.
  3. Kwenye sufuria nyengine katakata tomato, kitunguu,tia mafuta nusu mengine utatia kwenye spaghetti.
  4. Weka jikoni ongeza thomu,tomato ya kopo kijiko kimoja na pika kwa nusu saa.
  5. Saga mchanganyo wa mboga ulopika kwa machine ya kusagia (handy mixer); paka isagike kisha ongeza tena tomato ya kopo ilobakia usisage tena hapa.
  6. Rojo lile la mboga, mimina nyama changanya na rudisha kwenye jiko kwa moto wa chini na iache ipikike kwa muda wa dakika 45 – 50; Na sosi itakuwa tayari.

Spaghetti

  1. Sufuria ya nafasi tia maji weka katika jiko yaache mpaka yachemke kisha mimina spaghetti.Ziache mpaka ziive  toa moja ubonyeze ukiona imewiva ,chuja maji yote.
  2. Rudisha sufuriani kisha mimina chumvi na mafuta ulobakisha zipepete zichanganyike mafuta vizuri.Tayari kuliwa.

Kidokezo

Unaweza kukwaruza cheese kwenye spaghetti baada ya kupakuwa kama kwenye picha.

 

 

Share