Amehamia Nyumba Mpya Na Kumetokea Moto Baada Ya Usiku Wake Kusomwa Qur-aan, Ni Nini?

SWALI:

mehamia nyumba mpya imetokezea moto juu ya mlango,  na umetokezea kama  umesa ujiani ndani ya nyumba baada usiku kusomwa kuran, jee unaweza kuniambia kwa nini? nipo katika hofu,


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hatuwezi kujua sababu ya moto huo, huenda ikawa ni tatizo la umeme. Hakikisha tatizo hilo halipo. Usijitie wasiwasi sana, inatosheleza ukiwa utasoma Qur-aan na nyiradi za asubuhi na jioni na nyinginezo kujiepusha na kila shari na balaa. Bonyeza viungo vifuatavyo upate du'aa za kukuhifadhi Inshaa-Allaah.

 

Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

Anachosema kwa ajili ya kurudisha (kuzuwia) vitimbi vya mashetani wabaya.

 

Kisha soma Swali na Jibu lifuatalo upate maelezo ya kuhamia katika nyumba mpya lenye du'aa na nyiradi za kusoma:

Unapohamia Katika Nyumba, Unatakiwa Usome Au Kufanya Chochote 

 

Tunakuombea kila la kheri katika nyumba yako mpya, kheri na Baraka.

 

Na Allaah Anajua zaidi

  

 

Share