Kuwagharimia Wazazi Kwenda Hajj Kabla Ya Kufanya Mwenyewe

 

Kuwagharimia Wazazi Kwenda Hajj Kabla Ya Kufanya Mwenyewe

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali La Kwanza:

 

Assalamu Aleikum,

 

 

Swali langu ndugu yangu muislamu ni hili.mimi naishi Holland Europe na nina azma ya kumpeleka mamangu Hajj na mimi bado sija Hiji. Je naweza kumpeleka mamangu kabla mimi mwenyewe kuhiji??

 

 

Swali La Pili:

 

If my Son, want to send me for Hajj ( he is the one paying the ticket for me ), na yeye bado hajenda, wala haja plan when to go. He wants me to go , because i am getting old, nguvu zimekwisha na Umri kama bado nitakuwa niko duniyani, etc.

 

Nimepata jibu kwa mtu  that one of the Sheikh's said that mtu mpaka ende yeye Hajj, halafu ndio ataweza kumpeleka mtu mwengine. Lakini, he is paying for my Trip for Hajj, because mimi sina mume wakunipa pesa zakwenda . Na mimi sifanyi kazi, kwa hivyo sina uwezo wa kupata ticket ya safari ya Hajj. Naomba jibu kutoka kwenu 

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hija ni wajibu kwa kila Muislam aliyebaleghe na mwenye uwezo na akili timamu, hivyo basi, inahitajika kwanza wanaotaka kuwatumia gharama wazazi wao ili wafanye fardhi hii, wao kwanza waifanye ibada hiyo kabla ya kumpeleka au kumgharamia mwengine. Na kutoitekeleza fardhi hii bila ya udhuru itakuwa ni kumuasi Rabb Mtukufu na pia ni dhambi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾ 

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu. [Al-'Imraan: 97]

 

 

Ikiwa mtu ameweka nia kumpeleka mzazi wake Hajj kwa kumtumia gharama ili akaifanye mwenyewe, basi inaweza kukubalika ikiwa mtu huyo ana udhuru wa kutoweza kwenda mwaka huo. Ama kumfanyia Hajj mtu mwengine au kumgharamia na hali mwenyewe hakuifanya basi haifai hadi awe kwanza  mwenyewe keshaifanya.

 

 

Ifahamike kuwa kila mtu siku ya Qiyaamah atahukumiwa kwa 'amali zake na 'amali zake ndizo zitakazohesabiwa kwanza na si za wengine kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ﴿٣٨﴾وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ﴿٣٩﴾وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ ﴿٤٠﴾ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَىٰ ﴿٤١﴾

Na kwamba mbebaji dhambi hatobeba mzigo wa mwenginewe. Na kwamba insani hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi. Na kwamba juhudi yake itakuja kuonekana.  Kisha atalipwa jazaa kamilifu. [An-Najm: 38-41]

 

 

Wala hakuna yeyote atakayebeba dhambi au mema ya mwingine; si wazazi wala ndugu wala jamaa yeyote:

 

وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَىٰ حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَيْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۗ 

Na wala mbebaji yeyote hatobeba mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Na aliyeelemeshwa mzigo akiita ili kusaidiwa kubebewa mzigo wake, hatobebewa chochote, japokuwa ni jamaa wa karibu. [Faatwir: 18]

 

 

Vilevile hatujui mtu uhai wake una muda gani, lini atachukuliwa na Rabb wake.  Hivyo inahitajika zaidi mtu aharakishe kwanza kujifanyia Hija mwenyewe kabla ya kumfanyia mtu mwengine  hata ikiwa ni wazazi wake. Ile itikadi walionayo wengi wetu kuwa mama ni mkubwa kiumri na anaweza kuondoka kabla ya mwanawe, ni itikadi isiyo sahihi kwa sababu hakuna anayejua siku yake ya kufa na hakuna mwenye kujua ataishi umri gani,  kwani mauti hayana mdogo wala mkubwa.

 

 

Ushauri wetu ni kuwa, ikiwa hakuna kizuizi chochote cha mtu kufanya Hija mwaka huu, basi waharakishe wao  kuitekeleza   kwanza na waweke nia inshaAllaah mwakani kuwagharamia au kuwafanyia mzazi/wazazi.

 

 

Baadhi ya 'Ulamaa wamesema kuwa udhuru wa kukosa Mahram unakubalika kwa Mwanamke kutokwenda Hajj. Hivyo ikiwa hii ni hali ya muulizaji, basi anaweza kumgharimia mzazi wake kwenda Hajj kisha atakapopata tu yeye mahram atie nia ya kwenda.  

 

 

Na mama naye aliyekuwa hana uwezo kama ilivyokuwa hali ya muulizaji wa pili, basi naye hana wajibu wa kutekeleza Hajj kwani fardhi hii ni kwa wale wenye uwezo tu kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ 

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. [Al-'Imraan:97]

 

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

Share