Tofauti Baina Ya Masikini Na Fukara – Je Mkimbizi Yumo Katika Hali Hizo?

 

Tofauti Baina Ya Masikini Na Fukara – Je Mkimbizi Yumo Katika Hali Hizo?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nani maskini na nani fukara? Je, mkimbizi ni maskini au fukara? Allaah awafanyie sahali kwa kuyajibu maswali yetu yasiyoisha....amiin

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Takriban fakiri na masikini ni sawa sawa; wote hawana hali nzuri. Hata hivyo, fakiri hali yake ni mbaya zaidi kuliko hali ya masikini. Fakiri ni yule anayepata chini kuliko nusu ya mahitajio yake ilhali masikini ni yule anayepata zaidi kuliko nusu ya mahitajio yake.

 

 

Ama kuhusu mkimbizi anaweza kuwa katika mojawapo ya makundi hayo mawili. Na pia inawezekana kuwa mkimbizi akawa ni tajiri kwani alikimbia kutoka katika nchi yake kwa sababu moja au nyingine ilhali aliweza kutoka huko na pesa zake nyingi alizokuwa nazo. Kadhalika inategemea ni mkimbizi wa nini, wa siasa, au wa uchumi? Na pia inategemea yuko katika nchi ipi ambayo amehifadhiwa. Aliyepewa hifadhi Ulaya na Amerika hawezi kuwa sana na aliyepewa hifadhi Afrika.

 

 

Kwa mujibu wa wakimbizi walioko Ulaya na Amerika, wengi hawana shida wala tatizo lolote, na hawawezi katu kuingia katika fungu la umasikini wala ufakiri, isitoshe wengi ni wana uwezo mkubwa na hata kuitwa matajiri kulinganisha na watu wengi walioko Afrika.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share