Baba Aliyeoa Wake Wanne Amefariki – Naogopa Kudai Urithi

SWALI:

 

Assalam alykum warahmatullahi wabarakatuhu.

Swali langu ni hili.

Baba yangu kafaa mwaka 2000 na kaacha nyumba na alikuwa kaowa wake 4 sasa mimi na mama yangu hatueshi hapo tunaeshi kwao na mama na wao hawajifikirii kuhusu kugawa urithi na hata kunisaidiya mimi hawajifikirii, na hapo kwenye iyo nyumba alioacha baba anaeshi mama mkubwa na wanae na mimi ndio wa mwisho ninahofia kuomba urithi juu niko mdogo sasa nifanyeje na mnanishauri nini?


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hofu ya kudai urithi.

 

Hakika ni kuwa pindi mtu wa karibu anapokufa kama baba, mama, mke, mume inakuwa ni haki kwa warithi kupata urithi wao. Inapasa kwa wazee wanaobaki kuhakikisha kuwa kila mmoja amepata haki yake, na ikitokea kuwa mwenye haki kwa mfano kama wewe hujapatiwa mgao wako, basi sheria inakutaka uombe haki yako kwa njia nzuri.

 

Kwa ajili hiyo inafaa wewe na mama yako kuzungumza na jamaa kuhusu kupatiwa haki zenu nyinyi na wote ambao hawakupewa. Katika hali hiyo wake 4 watagawanya thumuni (1/8). Na ikiwa aliyefariki aliacha baba na mama wao pia watapata haki yao kwa alichoacha mtoto wao.

Tunakuombea kila la kheri katika kutafuta haki yako.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share