Kutumia Vyombo Vya Dhahabu Na Fedha Inajuzu?

 

 

Kutumia Vyombo Vya Dhahabu Na Fedha Inajuzu?

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

Swali:

 

Ama baada ya salamu natumai mnaendelea vema kwa uwezo wa ALLAAH KARIM. Swali langu ni kama ifuatavyo!! Je inafaa kutumia vyombo vya silver (fedha) na gold (dhahabu) kwa mfano kikombe au glasi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani? Tafadhali naomba mnifahamishe. Nawatakia kheri nyingi kutoka kwa ALLAAH na awafanyie wepesi katika kila jambo jema mnalolikusudia, wa hadha Assalam Alaykum Warahmatullah Wabarakat

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Ama Kiislamu utumiaji wa vyombo vya dhahabu na fedha haikubaliwi kabisa. Dalili ya hiyo ni Hadiyth zifuatazo:

 

 

1-Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anayekunywa katika chombo cha fedha anaangushia moto tumboni mwake” [al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

2-Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “… na ametukataza kuvaa pete za dhahabu na kunywa katika chombo cha fedha …” [al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

3-Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu)  amesema kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “… na msinywe katika chombo cha dhahabu na fedha, na msile katika sahani zake, kwani hivyo ni vyao duniani na ni vyetu Aakhirah” [al-Bukhaariy na Muslim].

 

Kwa hiyo, vyombo hivyo havifai kutumiwa na Waislamu ki-shariy’ah

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share