Skip to main content

Mkate Wa Shimari Na Zabibu

Mkate Wa Shimari Na Zabibu

Vipimo

Unga wa ngano 2 ½ Vikombe Vya chai

Siagi 3 vijiko vya supu

Chumvi 1 kijiko cha chai

Sukari 1 kijiko cha supu

Hamira 1 ½ vijiko vya chai

Bizari tamu (Shimari) 1 kijiko

Zabibu kiasi ukipenda

Yai 1

Rangi ya manjano kidogo tu

Baking powder 1 kijiko cha chai

Maziwa 1 kikombe cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia vitu vyote pamoja isipokuwa zabibu utatia kisha kanda.
  2. Kisha tia maziwa kidogo kidogo na huku ukikanda mpaka uwe laini kidogo utakuwa unashika.
  3. Halafu tia zabibu funika weka pembeni mpaka ufure (uumuke) kidogo.
  4. Kisha utauchanganya tena na utamimina kwenye sufuria na utautandaza kisha funika weka pembeni mpaka ufure zaidi.
  5. Halafu pakiza maziwa juu na choma kwenye oveni moto wa 350°c hadi iwive nakubadilika rangi juu.
  6. Epua na itakuwa tayari.