Maharage changa, Kamba Na Nudo (noodles)

Maharage changa, Kamba Na Nudo (noodles)

Vipimo

Maharage (mfano wa nyasi) - 1 chupa

Pilipili boga  nyekundu, kijani, manjano - 3

Nudo (noodles) - 2 pakiti

Kamba - 200g

Mafuta ya zaituni - 100ml

Chumvi - Kiasi

Vitunguu vya kijani - miche 5

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Osha pilipili boga, vitunguu katakata nyembamba.
  2. Vitunguu vya kijani vichane,ukate kate vyembamba vilevile.
  3. Weka sufuria ya nafasi tia mafuta anza kukaanga vitunguu,pilipili boga hadi zilainike kidogo.
  4. Maharagwe yachuje maji kisha mimina ndani ya mchanganyiko wa mboga uloanza kukaanga endelea kukaanga kwa moto wa kiasi paka zikaangike.
  5. Katakata kamba wawe vijipande vijidogo sana osha na kaanga kando mpaka waiive kwa kubadilika rangi.
  6. Chukua sufuria tia maji yachemshe mimina zile nudo pekee kwani kila paketi ndani  muna vijipaketi (extra)vijidogo vya chumvi,masala,mafuta usitumie vitu hivi.
  7. Nudo zikisha chemka kwa muda wa dakika mbili au tatu zichuje maji yote zimwage kwenye mchanganyo wa mboga uchanganye hadi zichanganyike.
  8. Sasa chukuwa wale kamba ulowakaanga umwagie juu na uchanganye vile vile na chakula tayari kwa kuliwa.

Kidokezo:

Unaweza kutumia kuku kidari bila mifupa,nyama yakusaga na huwa nzuri ukitayarisha saladi ya majani wakati wa kula chakula hiki.

 

Share