Mchuzi Wa Samaki Wa Salmon Wa Nazi

Mchuzi Wa Samaki Wa Salmon Wa Nazi

Vipimo

Samaki (salmon)- 2lb  

Kitunguu- 1 

Nyanya - 1 

Kitunguu saumu(thomu/galic)- 1 kijiko cha chai  

Bizari manjano- ½ kijiko cha chai  

Bizari ya mchuzi (curry powder) - ½ kijiko chai  

Kidonge cha supu- ½  

Mafuta- 3 vijiko supu  

Nyanya kopo - ½ kijiko chai  

chumvi -  kiasi  

limau - kiasi 

Pilipili nyekundu nzima -  2 

Nazi - kiasi  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Kata samaki vipande vya kiasi muoshe vizuri.
  2. Tia limau na chumvi kishaweka kando  
  3. Kaanga vitunguu mpaka viwe vekundu tia bizari ya mchuzi, manjano na    thomu
  4. Tia samaki kidonge cha supu funika kwa moto mdogo
  5. Halafu tia nyanya, nyanya kopo na pilipili funika tena mpaka ikaangike
  6. Kisha tia nazi wacha ichemke onja chumvi na ukamulie limau uwache  mpaka motoni mpaka uwe mzito kiasi na itakuwa tayari.

 

 

 
Share