Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Kukaanga Kwa Sosi Ya Nazi

Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Kukaanga Kwa Sosi Ya Nazi

 

 

Vipimo Vya Samaki Wa Nguru  

 

Samaki nguru - 5 vipande 

Kitunguu saumu (thomu/garlic) na tangawizi iliyosagwa- 1 kijiko cha supu 

Pilipili mbichi iliyosagwa - kijiko cha supu 

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi -1  kijiko cha chai  

Ndimu - 2 kamua maji 

Chumvi -  kiasi  

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki Nguru

 

  1. Changanya vitu vyote katika kibakuli ufanye masala ya kupaka kwenye samaki.
  2. Roweka kwa muda nusu saa
  3. Kaanga vipande vya samaki vikiwiva epua uchuje mafuta.

 

Vipimo Vya Mchuzi Wa Nazi Wa Sosi Ya Nyanya 

 

Vitunguu maji -  2 katakata vidogodogo

Nyanya -   3 saga au katakata ndogondogo

Tuwi zito la nazi - 2 vikombe viwili 

Haldi (bizari ya manjano) -  ¼ kijiko cha chai 

Pilipili mbichi - 1 isage

Ndimu - kiasi 

Chumvi -  kiasi 

Mafuta – vijiko 3 vya supu 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Mchuzi

 

  1. Katika sufuria tia mafuta kaanga vitunguu hadi vilainike.
  2. Tia nyanya ulosaga endelea kukaanga.
  3. Tia bizari, pilipili ulosaga.
  4. Tia tui kikombe kimoja koroga.
  5. Weka samaki katika chombo cha kupakulia kama bakuli umwagie sosi uchanganye bila kuvuruga samaki.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

 

Share