Mchuzi Wa Samaki Mgebuka (Herring)

Mchuzi Wa Samaki Mgebuka (Herring)

Vipimo

Samaki Mgebuka wa kopo (herring) -  400 gms.  

Vitunguu vilokatwakatwa - 3

Nyanya/tungule katakata-  5-6   

Nyanya kopo - 3 vijiko vya kulia

Bizari mchanganyiko au garama masala -  2 vijiko vya chai

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Kotmiri (coriander) ilokatwakatwa - 1 kikombe

Chumvi -  kisia

Mafuta -  ¼ kikombe 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Weka mafuta katika sufuria, kisha kaanga vitunguu mpaka vilainike na kugeuka rangi kidogo.

  2. Tia nyanya, chumvi, pilipili, endelea kukaanga kiasi dakika tano.

  3. Kisha tia nyanya kopo na bizari endelea kukaanga kwa dakika moja.

  4. Tia samaki kwa kumchambua nofu vipande vipande. Changanya vizuri.

  5. Weka maji kidogo sana kiasi ¼ kikombe tu.  Acha kidogo katika moto uchemke mchuzi.

  6. Tia kotmiri changanya vizuri, zima moto.

  7. Pakua katika chombo pambia kotmiri.

  8. Tolea kwa mkate au vya kuchemshwa kama viazi (mbatata), mhogo, viazi vitamu, ndizi mbichi, n.k 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 Kidokezo: Unaweza kutumia samaki aina nyengine wa nofu ikiwa herring hapatikani.

 

 

 

 

Share