Anapoharibu Mimba, Afanye Wudhuu Au Ghuslu?

SWALI:

 

Mimi nina swali langu moja je DAMU ya mimba iliotoka au kutolewa ikisha isha mwanamke hujipa udhu vipi samaha ikiwa kama swali litakua limesha ulizwa sana na wengine

 

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu cha kufanya mwanamke anapoharibu mimba.

Katika kuoga josho la janaba ima kwa kukatika kwa damu ya nifasi au damu ya mwezi mwanzo unaanza na kuchukua wudhuu kama wa Swalah. Baada ya hapo unaoga mwili mzima.

Hii ndio njia ya kuoga baada ya damu kumalizika.

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi

Ghuslu - Vipi Kukoga Janabah, Nifaas Na Hedhi

044 - Kuoga (6) Kuoga Mwanamke Janaba, Hedhi Na Nifaas, Na Kukausha Viungo Baada Ya Kuoga

045 - Kuoga (7) Masuala Yanayohusiana Na Kuoga

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share