Bajia Za Bilingani Na Sosi Ya Kijani

Bajia Za Bilingani Na Sosi Ya Kijani

Vipimo

Bilingani - 2 ya kiasi

Unga mweupe - ½ kikombe

Unga we semolina - ½ kikombe

kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha chai

Vitunguu vya majani (spring onions) katakata - ½ kikombe (chopped)

Pilipili manga - ½  cha chai

Haldi (bizari manjano/tumeric) - ½ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

*Sosi ya kijani ya kikolezo (seasoning) - 1 kijiko cha supu

Maji ya kuchanganyishia - kiasi

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

  1. Weka mafuta katika karai
  2. Osha bilingani kisha kata slesi za duara za kiasi
  3. Changanya vitu vikavu kwanza katika bakuli kisha tia maji uchanganye vizuri. Mchanganyiko usiwe mwepesi sana.
  4. Kisha tia vitu vilobakia kama thomu, sosi ya kijani ya kukoleza na endelea kuchanganya vizuri.
  5. Chovya slesi za bilingani katika mchanganyiko uingia pande zote mbili. Usichovye sana.
  6. Tia katika mafuta ya moto kisha ukaange na ugeuze pande zote mbili hadi igeuke rangi.
  7. Chuja katika karatasi ya kuchujia mafuta (Paper towel) kisha panga katika sahani na ikiwa tayari kuliwa na sosi ya ukwaju,  au nyinginezo.

Bonyeza kiungo upate sosi za kulia bajia:

Sosi Ya Ukwaju

Chatine Ya Mtindi Na Nanaa

*Sosi Ya Kijani Ya Kukoleza (Green Seasoning)

Vipimo:

Vitunguu vya majani (spring onions) - 1 msongo

Figili mwitu (celery) - 2 miche

Kotmiri (coriander) - ½ kikombe

Pilipili mbichi - 3

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katakata vitu vyote kisha tia katika  mashine ya kusagia (blender).
  2. Tia maji kama ¼ kikombe, saga hadi iwe laini. Ikiwa nzito ongeza maji lakini isiwe nyepesi sana.
  3. Weka katika chupa kisha hifadhi katika friji au freezer utumie kwa mapishi mengineyo kama mchuzi n.k.

 

Share