Buns Za Nyama Ya Kusaga (Aina Ya 2)

Buns Za Nyama Ya Kusaga (Aina Ya 2)

Vipimo

Mayai - 4 
Mafuta- 1 kikombe

Maziwa - 1kikombe

Chumvi - kiasi

Hamira-  1 1/2 kijiko cha supu

Unga - kiasi 
Habat suda( blackseed)- 1 kijiko cha supu

Nyama yakima  kiasi  ipike kama ya sambusa

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kwenye  chombo kikubwa changanya mayai, mafuta, maziwa, chumvi changanya vizuri
  2. Tia hamira na habat suda kisha mimina unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko ushikane uwe laini.
  3. Iwache  ifure,ukisha fura kata madonge ya kiasi ujaze nyama katikati  kisha ufunge  iwe duwara  panga  kwenye sinia  kisha yapake maziwa kwa juu
  4. Choma  kwa moto wa 350  mpaka  zibadilike rangi na yawive  vizuri .
  5. Iwache ipoe  kisha  itakuwa tayari kuliwa .

Kidokezo: unaweza kujaza feta cheese na zaituni badala ya nyama  pia inakuwa nzuri .

 

Share