Vikate Vitamu Vya Vya Jibini, Ufuta Na Habbat Sawdaa

Vikate Vitamu Vya Vya Jibini, Ufuta Na Habbat Sawdaa 

  

Vipimo

  

Unga wa ngano - 4  vikombe

 

Yai -  1

 

Maziwa -  2  Vikombe  

 

Siagi -  ¼  Kikombe 

                                                         

Sukari - 2 vijiko vya supu

 

*Hamira -   1 ½ kijiko cha chai

 

Chumvi -    ¼ kijiko cha chai

 

Mjazo:

Jibini ya vipande -   kiasi

Ufuta  na *habbat sawdaa  (habba soda/black seeds) - kiasi

Yai la kupakia au maziwa ya kopo

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika. 

  1. Pakaza siagi treya ya oveni kwa ajili ya kupikia vikate.
  2. Tia unga katika bakuli, siagi, yai, maziwa, sukari, chumvi.
  3. Tiia *hamira  ya instant (kuumua moja kwa moja) au ikiwa ya kawaida, roweka katika kikombe chenye maji kidogo.
  4. Changanya vizuri ukande kidogo kidogo kiasi cha kuchanganyika.
  5. Tengeneza viduara, kisha sukuma kidogo utie kipande cha jibini na nyunyizia ufuta na habba sawdaa.
  6. Kunja pembe moja iungane na pembe ya pili, kisha chukua uma (fork) ubanebane ili ifungike.
  7. Vipange katika treya ya oveni
  8. Piiga yai moja katika kibakuli kidogo au tumia maziwa ya kopo ya chai, kisha tumia brush kwa ajili ya kupakaza juu ya vikate.  Nyunyizia ufuta na habba sawdaa.kisha viache viumuke.
  9. Wakati unasubiri viumuke, washa oven moto 350°. Kisha vikiumuka    choma (bake) katika oveni  kwa muda wa dakika 25-30. Vikiiva epua vikiwa tayari.

 

Kidokezo:

Habba sawdaa  ukipenda tu si lazima, unaweza kutia ufuta pekee.

 

 

 

 

Share