Maulidi: Anataka Kujua Kuhusu Maulidi Na Ikiwa Yameanzishwa Na Mashia

 

Anataka Kujua Kuhusu Maulidi Na Ikiwa Yameanzishwa Na Mashia

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

mm nimeshangwaza na hii kuhusu kua maulid wameyaanzisha mashia hivi ni kweli au kwa kua ndio mashia ni wabaya kama wanavyosema watu na ni makafiri tena iwe kila jambo kutupiwa wao. kwani mm nimesoma tarekhe zote mbili za kishia na za kisuni lakini kila mmoja hakusema kama suniy ndio alieanzisha au sunny kusema mashia ndio walioanzisha leo hii nyinyi ndio mnasema kua mashia ndio walioanzisha basi mm nataka hicho kitabu ambacho kinachosema kua mashia ndio walioanzisha maulid na nipeni adres ya kitabu na kila kitu kwani sasa ulimwengu umekua na kila mtu anavunia kwake sasa nami sitaki kua kesho masuli kwa mugu nataka kujua kila kitu .na si kama nawapenda mashia lakini mapaka sasa nasoma kote kote kwenye ushia na usuni kwani nataka kujua haki iko wapi? sina mengi ila andapo mkinijibu suali langu basi nitakua na mengi zaidi.  

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwa ujumla sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (Mawlid) zimeanzishwa kwa sababu na malengo tofauti na kwa madai tofauti. Watu wote hawa walioanzisha na wanaoadhimisha, wanadai kuwa wanampenda Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Miongoni mwa yenye kuthibitsha madai yao kuwa wanampenda Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni huku kumuwekea siku maalumu na kufanya wayafanyayo bila kujali kama Uislamu unayakubalika au kinyume chake, huku wakielewa fika kuwa walikuwako waliompenda Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao waliomuona na walioishi nae kabla yao na hawakuwa wakifanya hayo wayafanyanyo wao.

 

 

 

Kwa maelezo zaidi kuhusu asli ya Mawlid na waliyoyaanzisha soma makala hizi utazame na rejea:

 

Mawlid – Historia Yake, Hukmu Na Kauli Za ’Ulamaa

 

Mawlid (Kusherehekea Kuzaliwa Kwa Mtume)

 

Hukumu Ya Kusherehekea Kuzaliwa Kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

 

 

Hata hivyo, la kuzingatia na hili ndio tulielewe kuwa wote hao wawe Mashia au wengine wo wote wale ni wabaya kwani walichokifanya au wanachokifanya kwa visingizio vyote walivyonavyo; kwani kama kuadhimisha siku ya kuzaliwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni katika dini kwa maana ni ‘Ibaadah, ambalo ni jambo la kumkurubisha mtu kwa Rabb wake basi ni vyema tuelewe kuwa kufanya hilo kunatuweka kati ya moja katika mambo matatu; hasa hasa kwa kuwa kuadhimisha siku inayosemwa kuwa amezaliwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni katika yaliyothibiti kuwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na Salafus Swaalih na watu wote wa karne tatu bora za umma huu hawakuwahi kuadhimisha wala kufanya chochote chenye kuashiria kuwa kuna cha kufanywa katika siku hiyo kama ni maadhimisho.

 

 

Hivyo basi hao wafanyao mawlid wawe Mashia au wengine wowote wale wenye kufanana nao na wafanyao jambo lolote la kujikurubisha kwa Allaah ‘Ibaadah’ lisilothibiti, tuelewe kuwa huenda yakampelekea mtu kuwa nje ya duara la Uislamu kutokana na haya mambo matatu:

 

 

1. Mfanyaji huwa anathibithisha kwa vitendo vyake - kwa kufanya hilo jambo – kuwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakubalighisha  hakufikisha kikamilifu  alichotakiwa akibalighishe na  Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 

Lakini Muislamu hategemewi kufikiria hili achilia mbali kulithibitisha kwa vitendo vyake, hivyo.

 

 

2. Mfanyaji huwa anathibithisha kwa vitendo vyake kuwa yeye anaelewa zaidi dini, anamuelewa zaidi Muumba – mwenye kumcha Allaah - na anaelewa zaidi namna ya kujikurubusha kwa Rabb kuliko Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Lakini Muislamu hategemewi kufikiria hili achilia mbali kulithibitisha kwa vitendo vyake, hivyo.

 

 

3.   Mfanyaji huwa anathibithisha kwa vitendo vyake kuwa Qur-aan au Allaah – na tunajikinga kwa Allaah hakuwa mkweli Aliposema kuwa: Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. Basi atakayelazimika katika njaa kali bila kuinamia kwenye dhambi basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu Al-Maaidah: 3.

 

 

Lakini Muislamu hategemewi kufikiria hili wachilia mbali kulithibitisha kwa vitendo vyake, hivyo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share