Spaghetti Ya Sosi Ya Nyama Ya Ng’ombe Ya Kusaga Na Zaytuni

Spaghetti Ya Sosi Ya Nyama Ya Ng’ombe Ya Kusaga Na Zaytuni

 

Vipimo 

Spagetti paketi 1 ya 400 gms

Nyama ya kusaga ¼ kilo

Nyanya 3

Kitunguu 1

Mdalasini wa kijiti 1

Nyanya ya kopo vijiko 3 vya kulia

Tangawizi mbichi na thomu (garlic/saumu) ilokunwa au kusagwa vijiko 2 vya kulia

Chumvi kiasi

Pilipili manga kijiko cha chai 1

Oregano (aina ya herb ya Italy) kijiko 1 cha chai

Zaytuni (Olives)

Siagi vijiko vya kulia

Mafuta ya zaytuni (olive oil)  ¼ kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha spaghetti kwa muda wa dakika 20 kisha mwaga maji uchuje. Weka kidonge cha siagi ili yasigandane kisha weka katika sufuria ya kupashia chakula (hot pot).
  2. Osha nyama kidogo kisha changanya katika sufuria pamoja na tangawizi, thomu, pilipili manga, mdalasini, chumvi, na weka kidonge cha supu au supu ya nyama kidogo. Weka ipikike katika moto
  3. Tia nyanya zilosagwa endelea kupika kisha weka nyanya kopo, endelea kidogo kupika iwe sosi.
  4. Weka mafuta ya zaytuni na oregano .
  5. Epua weka katika hot pot, pakua katika sahani tolea kwa zaytuni na parsley (kotimiri mwitu)  

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share