Anaomba Majibu Kwa Dr. Paul Hamisi Hussein Kwa Hotuba Yake Iliyosema Uislamu Ni Dini Ya Majini

 

Anaomba Majibu Kwa Dr. Paul Hamisi Hussein Kwa

Hotuba Yake Iliyosema Uislamu Ni Dini Ya Majini

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam aleikum warhamtullahi wabarakatuh.

Mimi na ishi Holland,niko kijana wa myaka 12.

Swali langu nihili,nileweza kuona kwenye website ya www.youtube.com ambao niligunduwa Dr Paul Hamissi Hussein nalikuwa ana hutubiya mjini Rwanda-Kigali yakuwa Islam ni dini ya majini, na yeye ni mwenye asili yakutoka mjini Kigoma-Tanzania, je ndugu zangu wa Islam wa Alhidaaya hii mnaweza kuwa mlikwisha ona gisi nalivyo chafuwa dini ya kislam? Namengineyo mengi machafu nakuji tambulisha kuwayeye alikuwa sheikh waki Islam tunaombeni Alhidaaya hii tunaomba kwajili ya Allah muweze kumjibu kupitiya kwenye website ya www.youtube.com ili tuweze kufanikiwa tuone ukweli ili ndugu zetu wapate faida yakujuwa ipi dini ya haki? Na tunamuomba Al hadji Dr Soulley kutoka Tanzania aweze kutupa uwazi kwenye website hii www.youtube.com.

Wahadha Assalaam aleikum,tunawatakiya kila la kheri

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Tumetazama video zake kadhaa na yafuatayo ndio tumeyagundua:

 

  1. Ni mtu muongo.

 

  1. Haujui Uislamu kama anavyodanganya watu wengi ambao wanadhani anaujua Uislamu kwa kusema maneno ya Kiarabu bandia na kunukuu Aayah za Qur-aan huku akichanganya na maneno yake ya Kiarabu kisichoeleweka.

 

  1. Ananukuu Aayah za Qur-aan na kuzichanganya na maneno yake au na maneno ya biblia. Ukimsikiliza akitaja Aayah, basi fungua Msahafu na usome utaona anatoa maneno mengine yasiyokuwemo katika Qur-aan.

 

  1. Anatafsiri Aayah anazosema ni kutoka kwenye Qur-aan anavyotaka yeye ili kupotosha watu.

 

  1. Lugha ya Kiarabu anaikosea sana na kutamka vibaya na kutoa tafsiri kinyume.

 

  1. Ni wepesi kwa yeyote yule kumgundua kuwa ni mtu muongo kwani maelezo yake anayotoa mengi hayapo na mengine anatunga.

 

  1. Kasema kasoma Libya, Iran, Kuwait na Saudia, na yote ni uongo hakuna ushahidi wowote wa hayo.

 

  1. Kasema katumwa awe Shekhe wa Afrika ya Mashariki na maraisi au viongozi Khomeini, Saddam, Yasir Arafat na Qadhafiy (Gadafi) katika mkutano wa kumtawaza uongozi na kumpa cheti… na yote hayo ni uongo mtupu kwani viongozi wote hao wote hawakuwahi kukutana pamoja katika Historia. Isitoshe itikadi zao ni tofauti na hawasimamii Uislamu. Khomeini alisimamia Ushia na sio Uislamu. Wengine hawakuwa wanashughulika na dini hadi kufikia kumtuma mtu awe kiongozi wa dini. Utaona kuwa huyo muongo hajui hata kupanga uongo wake.

 

  1. Anaonekana ni mtu mjanja katumia hila zake hizo nyepesi kuwahadaa wagalatia ili apate maslahi yake ya kidunia. Na wajinga ndio waliwao.

 

   10. Kuna mashaka kama kweli alikuwa Muislamu. Na haitoshangaza kama mtu anadai  alikuwa Muislamu na wakati alikuwa Muislamu alikuwa ni mshirikina kama anavyojielezea mwenyewe, na haishangazi kutokuwa na matendo ya Kiislamu ikiwa kweli alikuwa Muislamu.

 

   11. Utagundua kuwa ujanja wake huo utakuta anakwenda kuufanyia huko Burundi na Rwanda na sio Tanzania alipotoka kwani wengi watamgundua uongo wake na ataumbuka mara moja.

 

Hivyo, usipoteze wakati wako kwa mtu kama huyo, na wale usijishughulishe na kuacha kazi za maana za kujieleimisha dini yako na kusikiliza watu kama hao wenye kutafuta pesa kwa wajinga wenzake ambao kila wanapomsikia mtu alikuwa Muislamu basi wanavutika kumsikiliza.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share