Mashairi: Nisikupende Kwa Nini?
Nisikupende Kwa Nini?
Muhammad Faraj (Rahimahu Allaah)
|
Ukiyaonja mapenzi |
utaujuwa utamu |
|
Ndipo utapoyaenzi |
ukayaona adhimu |
|
Nakupenda Mwenye enzi |
Ilahi Mola Karimu |
|
Nisikupende kwa nini |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Nisikupende kwa nini |
Ya Ilahi ya Karimu |
|
Nawe umenithamini |
kuniumba mwanadamu |
|
Ukaniongeza shani |
Kwa dini ya Isilamu |
|
Nisikupende kwa nini |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Meniumba insani |
Mwanadamu alo huru |
|
Ukanipa Qur ani |
Ili iwe yangu nuru |
|
Sasa nina kheri gani |
Kama sijakushukuru |
|
Kwa nini nisikupende |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Rasuli ukamtuma |
Ili aje nifundisha |
|
Kila jambo lilo jema |
Yote kanifahamisha |
|
Akafanya kila hima |
Risala kukamilisha |
|
Kwa nini nisikupende |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Akujuwaye yakini |
Hawezi kuwa mjinga |
|
Akamfwata shetani |
Na Wewe akakutenga |
|
Kwani vyote ardhini |
Asili yake mchanga |
|
Kwa nini nisikupende |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Umetuletea maji |
Twanywa tukiona raha |
|
Hujayafanya ujaji |
Machungu yenye karaha |
|
Ya Rabi ewe Mpaji |
Tuzidishie furaha |
|
Kwa nini nisikupende |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Mbingu ukaziumba |
Kwa nyota ukazipamba |
|
Na kisha ukaziremba |
Zikapangika sambamba |
|
Kama zimefungwa kamba |
Hapana kinachoyumba |
|
Nisikupende kwa nini |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Wallahi tukiperemba |
Kutizama utukufu |
|
Tunaelewa ya kwamba |
Ni kazi yako Latifu |
|
Ni kazi yako Muumba |
Ilo timu kamilifu |
|
Nisikupende kwa nini |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Neema zako ni nyingi |
Ya Rabbi l arbabu |
|
Umetupa mambo mengi |
Hayana hata hesabu |
|
Ewe Mpaji kwa wingi |
Ewe wangu Mahabubu |
|
Kwa nini nisikupende |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Hewa hii tuvutayo |
Moja ya Zako neema |
|
Neema ambayo kwayo |
Kukupenda ni lazima |
|
Lau kama hatunayo |
Uhai ungeyoyoma |
|
Kwa nini nisikupende |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Vyote ulitayarisha |
Hata bado kutuumba |
|
Mahitaji ya maisha |
Bila hata kukuomba |
|
Ukarimu usokwisha |
Kutoka kwako Muumba |
|
Kwa nini nisikupende |
Nawe Umenikirimu |
|
|
|
|
Ninakupenda Wallahi |
Na Wewe Ndiye Shahidi |
|
Pendo kwako likisihi |
Ndipo nitapofaidi |
|
Ninakupenda Ilahi |
Na Mtume Muhamadi |
|
Kwa nini nisikupende |
Nawe Umenikirimu |
