Saladi Ya Kukatwakatwa (Chopped) Na Parsley

Saladi  Ya Kukatwakatwa (Chopped) Na Parsley

Vipimo:

Kitunguu cha rangi ya zambarau - 2

Nyanya - 3

Kitunguu cha majani (spring onions) - 5   Miche (stalks)

Parsley  (aina ya kotmiri) - 1 msongo (bunch)

Pilipilipi boga (capsicum)  la kijani - 1

Pilipilipi boga (capsicum)  la jekundu - 1

Tango - 1

Sosi Ya Saladi (Salad Dressing)

Mafuta ya zaytuni - ¼ kikombe

Pilipili ya unga - 1 kijiko cha chai

Siki - 3 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilochunwa (grated) - 3 chembe

Changanya vitu vyote katika kibakuli

Namna Ya Kutayarisha Saladi

  1. Menya kitunguu na osha saladi na mboga zote weka kando.  Chuja maji parsley katika kichujio baada ya kuiosha.
  2. Kata vikonyo vya parsley  weka kando.
  3. Katakata vitu vyote vidogo vidogo katika mashine lake (chopper) au kwa mkono ukiweza.
  4. Tia katika bakuli,  na wakati kula tia mchanganyiko wa dressing yake uchanganye vizuri ikiwa tayari.

 

 

 

 

 

 

Share