Saladi Ya Majani, Karoti , Tango, Na Pilipili Mboga

Saladi Ya Majani, Karoti , Tango, Na Pilipili Mboga

 

Vipimo

Saladi la duara - 1

Matango - 2

Pilipili mboga jekundu - 1

Pilipili mboga kijani - 1

Karoti - 2

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katakata saladi la duara lioshe, lichuje na lipange katikati kwenye sahani.
  2. Katakata matango yapange moja juu la jingine kuzunguka sahani.
  3. Kuna (grate) karoti kisha mwagia juu ya saladi kisha katakata mapilipili mboga tupia tupia  juu ya karoti tayari kwa kuliwa.

 

Share